Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Maswali na majibu

Je, inawezekana kuambukizwa VVU kwa mwanaume kugusa

kwenye uke kwa vidole

Siyo rahisi kuambukizwa magonjwa ya ngono au VVU kwa njia hii, lakini

inawezakana. Kwa mfano, kama mwanaume ana shahawa kwenye vidole

na haraka sana akagusa kwenye uke. Pia kama ana kidonda au jeraha

kwenye vidole inawezakana VVU kupitia.

Je, VVU inawezekana kuambukizwa kwa kujamiiana sehemu ya

haja kubwa

Ndiyo. Ngozi ya ndani ya sehemu ya haja kubwa ni laini kuliko ngozi

iliyo ndani ya uke, na kuwa rahisi kuchubuka wakati wa kujamiiana.

Hivyo VVU inaweza kupitia kwenye jeraha na ni hatari kwa wenzi

wawili. Watu wanaojamiiana sehemu ya haja kubwa lazima kutumia

kondom.

Je, VVU inawezekana kuambukizwa kama mwanaume

akichomoa uume kabla ya kumwaga shahawa

Ndiyo. Hii siyo njia salama ya kuepuka VVU au majonjwa mengine ya

ngono. Kiasi kidogo ya shahawa inatoka kwenye uume kabla ya kumwaga

shahawa. Na pia majimaji ya uke inaweza kuingia kwenye tundu la uume.

Kondom tu ndiyo kinga imara ya VVU wakati ya kujamiiana.

Je, VVU inawezekana kuambukizwa kwenye choo

Hapana. VVU haiwezekani kuambukizwa kwenye choo.

Kwanini kondom inaweza kupasuka

Ukijifunza njia ya kutumia kondom kwa uhakika, siyo rahisi kupasuka

wakati wa kujamiiana. Ni wakati tu kondom haijavaliwa sawasawa ndipo

kondom inaweza kupasuka. Na ndiyo maana ni muhimu kufahamu jinsi

ya kutumia kondom sawasawa.

57 KISWAHILI