Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Jinsi ya kuishi na VVU

Kuna njia nyingi zinazo saidia walioathirika kuongeza muda wa kuishi na

afya njema, kwa mfano:

1. Kujifunza kuhusu VVU na ukimwi.

2. Kwenda hospitalini mara kwa mara kuzungumza na madaktari au

watoa ushauri kuhusu VVU.

3. Kutumia madawa ya hospitali (ARVs) zinazo saidia waathirika

kuishi zaidi.

4. Kutumia kondom kila tendo la ngono. Pia waathirika

wanapojamiiana pamoja ni lazima kutumia kondom, kwa sababu

kila mara wanapojamiiana bila kondom wanaweza kuambukizana

tena na inaweza kupunguza muda wao wa kuishi.

5. Kujipa matumaini na usiwe na hofu au wasiwasi.

6. Kuendelea kushirikiana na familia na jamii.

7. Kulinda mwili kwa kula vyakula bora kama matunda, mboga,

nyama na maziwa, na kufanya mazoezi ya mwili.

8. Kwenda hospitali au kliniki kila mara kutibiwa magonjwa

mengine haraka.

9. Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako. Uvutaji wa sigara ukiwa

na VVU inaweza kudhoofisha afya yako kwa haraka. Ni heri

kutovuta sigara.

10. Unywaji wa pombe ni hatari kwa afya yako. Unywaji wa pombe

ukiwa na VVU inaweza kudhoofisha afya yako kwa haraka. Ni

heri kutokunywa pomba.

11. Kutumia madawa ya kienyeji yanaweza kusaidia kutibu baadhi ya

magonjwa ya ukimwi. Lakini uwe mwaangalifu kwa watu

wanaodanganya kuwa wana madawa ya kutibu VVU kwa

sababu mpaka sasa hakuna tiba kabisa.

55 KISWAHILI