You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Elimu ya kupima VVU

Njia pekee ya kuweza kufahamu kama umeaambukizwa VVU ni kupima

damu tu kwenye kliniki au hospitalini. Huwezi kufahamu kwa kuangalia

mtu. Watu wengi wenye VVU huonakana wana afya na hawajui kama

wameathirika kwani hawajapima hospitalini.

VVU haina tiba kabisa. Mtu akiambukizwa VVU hakuna njia yoyote ya

kutoa VVU mwilini. Lakini siku hizi dawa (ARVs) zinapatikana

hospitalini zinazoweza kuongeza muda kutoka kuaambukizwa VVU hadi

kuugua ukimwi.

Watu wanaofahamu kuwa wameshaambukizwa VVU kabla ya kuugua

magonjwa ya ukimwi kawaida huishi muda mrefu kuliko wale

wanaofahamu baada ya kuugua. Kwa sababu hii, kupima na kufahamu ni

muhimu na inaweza kukusaidia kuwa matumaini na kuongeza muda wa

kuishi.

Kama utaamua kupima damu kwa ihari utapata nafasi ya kuzumgumza

pekee yako na daktari. Utapewa ushauri na daktari kusiana na VVU na

vipimo vyako vya damu. Daktari hatatoa kwa mtu mwingine maelezo ya

matokeo ya vipimo vyako.

49 KISWAHILI