Kielelezo Patanifu cha Katiba ya Kenya - ConstitutionNet
Kielelezo Patanifu cha Katiba ya Kenya - ConstitutionNet
Kielelezo Patanifu cha Katiba ya Kenya - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
JUMAPILI, NOVEMBA 22, 2009

KIELELEZO PATANIFU CHA KATIBA YA KENYA

Imechapishwa mnamo Novemba 17, 2009 na Kamati ya Wataalam Kuhusu Marekebisho ya Katiba Kulingana na

Sehemu 32(1)(a)(i) ya Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya Kenya, 2008.

39

(ii) kuwapa kazi walimu walioajiriwa na Tume kuhudumu katika

shule yoyote ya umma na taasisi nyingine.

(iii) kuwapandisha vyeo na kuwahamisha walimu;

(iv) kuwaadhibu na kuwadhibiti walimu;

(v) kuwafuta kazi walimu; na

(vi) kutekeleza majukumu mengine yaliyopewa Tume na Sheria

ya Bunge.

(3) Tume itachunguza viwango vya elimu na mafunzo kwa watu wanaojiunga

na taaluma ya ualimu na kutoa walimu na itashauri serikali ya kitaifa kuhusu

masuala yanayohusiana na taaluma ya ualimu.

Sehemu 3 – Huduma ya Marekebisho ya Kenya

Kubuniwa na kudhibitiwa.

278. (1) Kuna Huduma ya Marekebisho ya Kenya iliyobuniwa katika utumishi wa

umma.

(2) Malengo ya Huduma ya Marekebisho ya Kenya ni kuhakikisha –

(a) kwamba wafungwa katika magereza nchini wamehifadhiwa salama

na kwamba taasisi hizo zina mazingira yanayofaa binadamu kuishi

kulingana na Katiba na sheria;

(b) kuwasimamia wahalifu katika jamii ambao wanahudumu vifungo

vya nje au ambao wanachunguzwa; na

(c) kuwarekebisha wahalifu ili kuwaandaa kurudi na kuishi maisha yenye

manufaa katika jamii.

(3) Huduma ya Marekebisho ya Kenya itakuwa na muundo na kudhibitiwa ili

iweze –

(a) kufikia viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu miongoni mwa

wanachama wake na kupitia kwa wanachama hao katika kutekeleza

mamlaka yake;

(b) kukuza uwajibikaji na kuzuia ufisadi;

(c ) kuzingatia viwango vya haki za binadamu katika kutekeleza mamlaka

yake na utendakazi wa majukumu yake; na

(d) kutoa mafunzo kwa wanachama wake kufikia viwango vya juu vya

uwezo wao na kuhusiana na matumizi machache ya mabavu na kuwa

na uadilifu na kuheshimu haki za binadamu , uhuru wa kimsingi na

heshima ya binadamu.

(4) Huduma ya Marekebisho ya Kenya itaandaliwa kuhusisha muundo wa

ugatuzi.

(5) Bunge litatunga sheria -

(a) kubuni miundo ya kutosha kuwezesha utawala unaozingatia uwazi

katika Huduma ya Marekebisho ya Kenya;

(b) kuruhusu mpango, usimamizi na utendakazi wa Huduma ya

Marekebisho ya Kenya; na

(c) kwa jumla kudhibiti Huduma ya Marekebisho ya Kenya.

Mkurugenzi Mkuu

279. (1) Kuna ofisi buniwa ya Mkurugenzi –Mkuu wa Huduma ya Marekebisho ya

Kenya.

(2) Mkurugenzi – Mkuu atateuliwa na Rais wa Kitaifa, kwa ushauri wa Tume

ya Utumishi wa umma na baada ya kuidhinishwa na Bunge.

(3) Mtu atateuliwa kuwa Mkurugenzi- Mkuu iwapo mtu huyo ana sifa zifaazo

kitaaluma na –

(a) amehudumu katika Huduma ya Marekebisho ya Kenya kwa angalau

miaka kumi; au

(b) ana uzoefu mpana katika usimamizi na utendajikazi kuhusu

huduma za marekebisho.

(4) Mkurugenzi-Mkuu atahudumu kwa muhula wa miaka mitano na ataweza

kuteuliwa kwa kipindi kingine cha mwisho cha miaka mitano.

(5) Kifungu 297 (3) kuhusiana na sifa za kuajiriwa zinazohitajika na Tume

zitazingatiwa katika kumwajiri Mkurugenzi-Mkuu.

SURA YA KUMI NA SABA

Sehemu 1- Taasisi za Usalama wa Taifa

Kanuni na misimamo

280. (1) Usalama wa Taifa ni ulinzi wa mipaka ya Kenya, watu wake, mali yao,haki

na uhuru, na maslahi mengine ya kitaifa dhidi ya vitisho vya ndani na nje.

(2) Usalama wa taifa la Kenya utaimarishwa na kuhakikishwa kulingana na

kanuni zifuatazo –

(a) usalama wa taifa unaongozwa na mamlaka ya Katiba hii na Bunge;

(b) Usalama wa taifa utatekelezwa kwa kuzingatia sheria, ikiwemo

sheria ya kimataifa, na kwa kuheshimu kikamilifu utawala wa kisheria,

demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa kimsingi;

(c) taasisi za usalama wa kitaifa zitaheshimu tamaduni mbalimbali za

jamii nchini Kenya katika kutekeleza majukumu yake; na

(d) uajiri katika taasisi za usalama wa taifa utaakisi mseto wa watu wa

Kenya katika viwango sawa.

Taasisi za usalama wa taifa

281. (1) Taasisi za usalama wa taifa ni -

(a) Vikosi vya Ulinzi wa Kenya;

(b) Huduma za Taifa za Upelelezi; na

(c) Huduma ya Polisi wa Kenya.

(2) Lengo la kimsingi la taasisi za usalama wa taifa na mfumo wa usalama ni

kulinda maslahi ya watu wa Kenya na mali yao na haki na uhuru, na mamlaka

, amani, umoja wa kitaifa na mipaka ya Kenya.

(3) Katika utekelezaji wa majukumu yao, taasisi za usalama wa taifa na kila,

mwanachama wa taasisi hizo hataruhusiwa -

(a) kuwa na upendeleo kwa njia yoyote,

(b) kuendeleza maslahi ya chama chochote cha kisiasa wala sera zake;

(c) kuhujumu maslahi ya kisiasa au mpango wa kisiasa ambao ni halali

chini ya Katiba hii; au

(d) kutii amri yoyote isiyokuwa halali.

(4) Mtu hataruhusiwa kubuni shirika linalohusiana na usalama wa taifa au

shirika wa kijeshi isipokuwa inavyoruhusiwa na Katiba hii au Sheria ya Bunge.

(5) Taasisi za uslama wa taifa zitakuwa chini ya mamlaka ya raia.

(6) Bunge litatunga sheria kuruhusu kushughulikia majukumu, utaratibu na

usimamizi wa taasisi za usalama wa taifa.

Kubuniwa kwa Baraza la Usalama wa Taifa

282. (1) Kuna Baraza buniwa la Usalama wa Taifa lenye –

(a) rais wa taifa

(b) Naibu Rais wa taifa;

(c) Waziri Mkuu,

(d) Waziri anayehusika na ulinzi;

(e) Waziri anayehusika na mashauri ya kigeni;

(f) Waziri anayehusika na usalama wa taifa;

(g) Mwanasheria Mkuu

(h) Mkuu wa Majeshi ya Kenya;

(i) Mkurugenzi –Mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Upelelezi; na

(j) Inspekta-Mkuu wa Huduma ya Polisi ya Kenya.

Majukumu ya Baraza la Usalama wa Taifa

283. (1) Baraza la Usalama wa Taifa –

(a) Litaunganisha sera za humu nchini, za kigeni na za kijeshi kuhusiana

na usalama wa kitaifa ili kuwezesha taasisi za usalama wa taifa

kushirikiana kikamilifu;

(b) kutathmini na kuchunguza malengo, kujitolea ,na hatari kwa Taifa

kuhusiana na usalama wa nchi; na

(c) kuanzisha sera kuhusu masuala ya maslahi ya pamoja ya kiusalama

ya taasisi za kiusalama na kudhibiti taasisi hizo.

(2) Baraza la Usalama wa Taifa litatoa ripoti kwa Bunge kila mwaka kuhusiana

na hali ya usalama nchini Kenya.

(3) Baraza la Usalama wa Taifa linaweza kwa idhini ya Bunge –

(a)kupeleka wanajeshi nje ya Kenya kwa minajili ya –

(i)kutekeleza majukumu ya Umoja wa Mataifa ya kudumisha amani

pamoja na majukumu mengine; au

(ii) kuidhinisha wanajeshi wa kigeni kutumwa Kenya.

Sehemu 2 - Majeshi ya Ulinzi wa Kenya

Kubuniwa kwa Vikosi vya Ulinzi wa Kenya na Baraza la Ulinzi

284. (1) Kuna vikosi buniwa vya Ulinzi wa Kenya vinavyohusisha –

(a) Kenya Army;

(b) Kenya Air Force; na

(c) Kenya Navy.

(2) Mtu hatabuni kikosi cha majeshi au kundi lenye hadhi ya kijeshi isipokuwa

inavyoruhusiwa katika Katiba hii.

(3) Kuna Baraza la Ulinzi lililobuniwa linalohusisha –

(a) Waziri anayehusika na ulinzi ambaye atakuwa mwenyekiti;

(b)Naibu Waziri anayehusika na ulinzi ambaye atakuwa naibu

mwenyekiti;

(c )Mkuu wa Majeshi ya Kenya;

Katiba mpya, Kenya Moja