constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
101

uchaguzi irudiwe. Education iwe ni ‘O’ level na awe ni mtu ambaye anatabia nzuri. Na miaka yake nayo iwe 35 mpaka 75.

Hesabu ya kura ihesabiwe yote ya President, ya Local Authority na Parliament, yote ihesabiwe kwa station ile ambayo

imetupiwa, after six O’ clock. Kwa hivyo hii document nimepatia Commission to peruse it for further recommendation. Thank

you.Com. Ibrahim Lethome: Yeah ndivyo.

Com. Ibrahim Lethome: Asante. Mugo Mwaura. Mugo Mwaura ni weweInterjection:

(Inaudible)Com. Ibrahim Lethome: Nilikuwa nimekuita Haya endelea.Wilson Kimei:

Kwa majina mimi ni Wilson Kimei Meli. Kwa upande wa ardhi tumeachwa nyuma sana, tumefinywa na hatuna sauti.Com.

Ibrahim Lethome: Unapendekeza niniWilson Kimei: Tukipendekeza, kama Mbunge anashindwa na kuongea, awe

akiokota maoni kwa wananchi. Na wananchi wawe wakipewa ruhusa kuongea katika District, na watangaze siku ambayo

wataweza kutoa maoni yao. Tangu uhuru 1963 hakuna mapato tumepata. Mashamba hatukonayo, elimu hatujapata, maploti

hata ikigawanywa hatupati. Tunaona kama tumeachiliwa nje na serikali na tunaona tuko nje ya serikali. Operation ikiendelea

kufanywa, sisi hatuna uhuru kwa sababu tunalala watu watano hadi kumi katika nyumba moja, ambayo sio sheria Kenya.Com.

Ibrahim Lethome: Lingine.Wilson Kimei: Haya nikiondoka hapo, elimu iwe ikionekana ni ya bure. Hospitali iangaliwe, ili

madaktari wasifanye kazi mara mbili. Unakuta madaktari wengine wako private na bado wako kwa serikali. Halafu tena wako

na store ya kuuza madawa. Hata C.I.D wa Kenya kumbe hawafanyi kazi, kama wako. Na kama wako, wanaokota maoni ya

wananchi kuhusu wagonjwaCom. Ibrahim Lethome: Lingine.Wilson Kimei: Ya mwisho ni hali ya wild life katika Kenya.

Yaani katika Laikipia hii, tunaona kama hatitusaidii. Mandovu yanakula mahindi.Com. Ibrahim Lethome: Unapendekeza

niniWilson Kimei: Hata heri ndovu waondolewe Laikipia ili tuweze kuishi.Com. Ibrahim Lethome: Inaudible.Wilson

Kimei: Eh binadamu aishi.Hali ya forest. Kama si forest, hatungekuwa na uhai, na kama tunachunga huko heri Mzungu

mwenyewa aliye Kenya ahame, tupewe mashamba. Tuko squatters tunaelezwa tukate vipande kama uko na miaka ishirini.

Com. Ibrahim Lethome: Wazungu waondolewe mashamba yapewe Waafrika Wilson Kimei: Yeah. Com. Ibrahim

Lethome: La mwishoWilson Kimei: La mwisho. Kuna urithi ama kama mtu ameaga tunampeleka mortuary, mwiaka yote.

Siku gani tutazika halafu tuwe tukiona kaburi ilikuwa hii, ilikuwa ya babu.Com. Ibrahim Lethome:Unataka nini

(Inaudible) Wilson Kimei: Yaani upewe ardhi, halafu mtu akifa umzike hapo. Si ati unaenda

Municipality kila siku kila siku. Na ma-plot yakigawanywa, yaangaliwe na serikali. Si ati mtu mmoja anapeleka. Pengine ni

mtu wa DP, anapewa mia na anauza. Pengine ni ya Kanu anauza na raia wanakosa. Com. Ibrahim Lethome: Unataka aje

Wilson Kimei: Kama DP inapewa kiwango fulani, iangikwe DP imepewa kiwango fulani. Na iandikwe namba mpaka

mwisho. Si ati mtu mmoja anyakuwe yote.Com. Ibrahim Lethome: Basi kuwe na balancing.Wilson Kimei: Yaani balancing

nikiona kama kamati ya Council iwe akitazama, ni bora. Lakini si ati ukifika Council hata uulize unaambiwa toka hakuna nafasi.

Ni kama wengine hatuna uhuru. Kwaherini.

Com. Ibrahim Lethome Mugo Mwaura yuko Charles Matheri Jacob Gichini Maigua Karibu. Halafu afuatwe na

Onesmus Karimu Njungwa kama yuko. Ni wewe Mzee Haya mtafauatana hivyo. Dakika mbili mbili. Jacob.Mary Wanja

Kamau: Mimi naitwa Mary Wanja Kamau na ningetaka kuchangia sana habari ya uwezo wa President. President ana uwezo

mkubwa sana ni ndio naona hata kwa hii nchi yetu mambo yanaharibika. Kwa mapendekezo yangu ningetaka President

aondolewe mamlaka ya kumchagua Permanent Secretary. Na tena aondolewe mamlaka ya kuwachagua judges na hata