12.07.2015 Views

Read - Al-Faqeer

Read - Al-Faqeer

Read - Al-Faqeer

SHOW MORE
SHOW LESS
  • No tags were found...

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Na aidha kwa Uongofu wa Mnyezi Mungu, ni yeye tundiye anayejua nani na nani aongoke au laa. Hii ni kwasababu Mnyezi Mungu hashirikiani na kiumbe yeyote katikakupitisha mambo yake – yeye hufanya apendavyo –haingiliwi hahojiwi wala hazuiliwi katika kupitishaayatakayo.Ikiwa ni hivyo basi kiumbe ana haki au wajibu wakuridhia juu ya kadhwaa ya Mnyezi Mungu na kuwekamatarajio na matumaini katika rehma zake kubwa mnozisojua mipaka. Na kwa vile Uislamu ni kusalimu amri nakunyenyekea kwa kadiri ya uwezo wake, basi mtuakiwafikishwa katika Uongofu basi la wajibu ni kuzidishaunyenyekevu wake na kuzidi kumuomba Mnyezi Munguambakishe Uislamuni na kumfariji kwa Husunul kha –tima asione kuwa kuswali kwake na kadhalika kutokana nauhodari wake katika kutumia nafasi ya ufinyu wa hiyarikuliko kua amependelewa kheri na Mnyezi Mungu.Mnyezi Mungu ni: Muqallibal Qullub. Mwenyekuzipindua nyoyo atakavyo, leo hivi kesho vile basiusijitukuze eti kwa sababu uko kwenye twa-a ya Mola wako,wala usimlaani na kumcheka ambae yuwamuhasi MnyeziMungu badala ya kumuombea Uongofu ili aongokewe kamawewe – kumbuka ya kua Mnyezi Mungu amemficha waliiwake baina ya watu, kwa hivyo si rahisi kumjua yuleunaemdharau yu vipi mbele zake Sub-hana wa Taala.Kama alivyoficha ridhaa yake katika Twa-a yake;na machukio yake katika maasi yake. hawezi mtu kujua niTwa-a gani anayoifanza ambayo itamridhisha MnyeziMungu au maasi gani anayofanza ambayo yatamchukizaMnyezi Mungu kwa hiyo asidharau thamma asidharau katikaTwa-a kitu chochote wala katika maasi kitu chochote.Kwa hiyo tumuombe Mnyezi Mungu atuwafikishekatika kheri zake, na katika yale anayoyapenda nakuyaridhia. Mambo yake mtu yote yameshaandikwa siku ileya kupulizwa roho akiwa ndani ya tumbo la mama yake:Riziki yake, Amali yake, Ajali yake, na kua kwakeMwema au Shakiyyi- yaani Muovu – (hadithi mashuhuri).Lakini Mnyezi Mungu ni mrehemevu na msamehevu kupitakiasi hakuna wa kuweza kukadiria. Na hakuna dhambiinayomshinda kusamehe – Illa-shirk. Basi tusikate tamaana rehema zake.WABILLAHIT - TAWFEEQ.17

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!