constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Hata nyinyi watu wa Wangige nyote si munajua hivyo? Simunajua River side? Hata tukichukua hawa, si tunaweza kuwapeleka

River side, hakuna mtu hajui hiyo, kwa hivyo chief aondolewe kabisa asante.(clapping)

Com. Wambua: Asante sana, tutamuita Robert Chege.

Robert Chege: Habari zenu, kwa majina ni kama hayo mumesikia. Nimetoka kijiji cha Gathiga. Mimi nashukuru kwa vile

mengi yametajwa hapa, ijapokuwa nataka kugusa tu mambo ya Commissioners. Hilo ni jambo langu la kwanza, kwa sababu

tunaongea mambo ya kutengeneza Katiba yetu sisi wa Kenya. Kuna maswali ingine huwa sisi wa Kenya tunajiuliza, kulingana

na vile sisi huwa tunaona.

Ya kwanza, ni kwa nini wakati sisi tumeitisha Katiba, ndio tunaletwa Commissioners, wale watakuja kutengeneza Katiba. Na

kulinga na maoni yangu, mimi naonelea katika Kanu, ndio tulipata Commissioners wengi. Ilehali katika total votes, zile tuko

nazo katika Kenya. Wako na less votes kuliko party zile zingine katika hii Kenya. Tena kuna wrangles, katika commision yao.

Unasikia kuna political interference, na mambo mengine mbaya, ambayo huwa inaendele tunasikia katika media. Tena hawa

makamishna huenda offisi kwa offisi, na hali hawaendi nyumba kwa nyumba. Kwa hivyo inaonekana, kuna kitu kile wana

serve, katika hii mambo ya kumaliza hii Katiba yetu. Tena tunambiwa Katiba itamalizika by December. By whose mandate, na

Katiba hii ni yetu? Hii Katiba ni sisi tulipatiwa conference, tuende tulizwe ile siku, Katiba hii tumetaja tunataka imalizike. Kwa

hivyo hapo tunaona tena kuna kitu ndani yake imefichwa. Tumeona kama hii Katiba haitafanyika kulingana na vile raiya

wanatoa maoni yao, tutaitisha further reforms kwa miaka ingine kama kumi na tano.

Nikiguza kitu kidogo mambo ya Presidency. President anafaa kuwa na powers, kuwa anapata ile mambo yote inatendeka

katika bunge anapitisha. Hafai kuwa juu ya sheria. Na hiyo basi anafaa kufutiliwa mbali katika bunge. Thus, we can have a

vote of no confidence from the Parliament, kama akipatikana na makosa yeyote. He should be of Kenyan origin. Awe na

miaka 35 mpaka 70. Awe mtu amefikisha form four and above, na awe na sound mind. Awe ameoa, na awe akitumia bidii

yake pahali inafaa. Awe mtu anajua mambo ya Mungu, na awe sio mtu ambae amehusika na mambo ya corruption, na awe

anadeclare wealth yake, wakati anasimama kwa Presidency. Tuwe na President and Vice President wawili.

Parties: Vyama nazo katika Kenya, ndio tusiwe na mambo ya ukabila, tuwe na vyama vitatu peke yake, katika Kenya yetu.

Na kuwe na serikali ya muungano, ambayo the winning party, huyo President, awe na over 50% total votes, na wa pili awe ni

wa chama hiyo ingine, awe ni first Vice chairman. Wa tatu ni wa chama hiyo ingine, awe second vice chairman.

Kusiwe na mambo ya merger anymore katika Kenya. Kwa sababu mambo ya merger inaleta dictatorship, ina kuja

ku-neutralize wale ma MP wengine wamekuwa swallowed. Hivyo basi, hawana nguvu ya kuongea kwa vile tayari wako chini

ya mtu mwingine.

51