12.07.2015 Views

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS
  • No tags were found...

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

21adhabu kali wala hakuna faini. Kuna wengine maanaka ni matajiri wataweza kutoa faini Kesi ya kunajisiwa iangaliwe auizikiliswe na askari mwanamke, hatutaki askari wa kiume.Mlalamishi asitishwe na wala asidharauliwe mahakamani.Haki za watoto – watoto waelimishwe kutoka shule za mzingi mpaka mwisho. Iwe ni lazima kwa akina mama. Mama ambayehatamsomesha mtoto wake au ambaye hatamuelimisha mtoto wake, achukuliwe hatua serikalini, na yule mtoto pia achukuliwehatua serikalini. Elimu iwe bure kwa watoto. Matibabu yawe ya bure kwa watoto, tunasumbuka sana sisi huku. Watotowasiozeshwe wakiwa wadogo. Mama yeyote au baba yeyote atakayeweza kufanya hivyo achukuliwe hatua serikalini, naadhibiwe vikali sana. Kwa sababu ni matatiso sana huku Lamu. Watoto wasifanyishwe kazi wakiwa wadogo – under age -.Mtoto wa kike na wa kiume waelimishwe sawa. Haki za watoto, wanaobandikwa mimba wakiwa wadogo, sikilizeni vizurisana. Mtu yeyote mwenye kumtia mtoto mdogo mimba alazimishwe aozwe. Kisha, ingine, amtunze mtoto kwa mahitaji yoyotebaada ya yule mtoto kuzaliwa sasa, amtunze kwa mahitaji yeyote muhimu: nguo, chakula na matibabu, mpaka afikishe miakakumi na nane – 18 years.Haya, ummasikini wa akina mama - namna ya kuondoa ummasikini. Akina mama wasaidiwe katika makundi ili wajiendeleze.Akina mama wapatiwe mikopo katika vikundi ili wajiendeze. Akina mama wahusishwe katika kazi mbali mbali.Haya, watoto mayatima hasa walioachwa na mama zao kwa sababu ya ukimwi: serikali ichukue jukumu kuangalia mayatimakwa chakula, elimu, matibabu na nguo. Serikali iwajengee mahali pa kuangalia hawa watoto mayatima.Wajane – wajane wenye ukimwi wahurumiwe, wapewe matibabu, chakula na nguo.Haya, ndoa ya lazima – Mwenye kumuoza mtoto wake kwa lazima ahukumiwe kisheria, yaani hatutaki ndoa ya lazima. Ndoaya lazima isiweko kabisa.Bunge – Viti vya maluu vya wabunge na ma-councillor wapewa wanawake. Kwa sababu kule bungeni tayari wanaumewametuzidi. Kwa hivyo viti hivyo twaomba kama wanawake wapewe nani, wapewe wanawake.Uwazi na uwajilikaji – wanawake wawekwe mstari wa mbele kujulishwa mambo yanaoendelea serikalini na majumbani. Mtuwa kwanza kujulishwa awe ni mwanamke.Tabia ya kuwanyanyasa akina mama katika miji: Mwanaume yeyote yule atakayempiga na kumjeruhi mwanamke, achukuliwehatua serikalini.Na Katiba iandikwe kwa lugha ya Kingereza na Kiswahili. Katiba ifundishwe mashuleni ili watoto wajue haki za nchi yao. MaAsalaam.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!