12.07.2015 Views

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS
  • No tags were found...

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

52(inaudible) Sio serikali yafaa kulinda dini.Kifungu cha tisa Bwana Chairman – Umilikaji wa Ardhi: swala la ardhi huwa ngumu sana hapa kwetu Kenya. Kwa sababulimeleta matatizo mengi na mafaa. Tatizo katika sehemu nyingi mbali mbali za nchi yetu ya Kenya ni ardhi. Ukosefu au uchachewa ardhi kwa watu wengi umekuwa tatizo sugu la wananchi weng, hasa wananchi wa mukoa wa Pwani. Kwa mfano katikakisiwa chetu cha Faza island, ambacho hata watu wengi hawajui kijiji chenyewe kinajulikana kama Faza Island. Hii ni sehemuyenye mashamba mengi yenye rutuba na mazao na majumba vitu naya zamani. Kwa muda wa miaka takribani elfu mbili nazaidi. Wenye kijiji hiki hawana kazi inayotambuliwa na serikali. Na hawa, wanyukusaji wanaitwa (inaudible) kwa hivyo sisi nimaskwota katika ardhi yetu.Bwana Chairman kifungu cha kumi - Mahakama ya Kadhi: kuhusu mahakama, kadhi mkuu awe na Kadhi’s High Court.Kadhi awe na mahakama ndogo au katika kiwango cha daraja ya Chief Magistrate. Kadhi mkuu awe nadaraja ya Judge waHigh Court. Kadhi yeyote awe na uhuru ya kusikiliza kesi yeyote kulingana na uwezo wake. Kesi ikiamuliwa na mahakamandogo ya Kadhi, inaenda appeal kwa mahakama makuu ya Kadhi. Mumeelewa?Com. Mosonik: Tumeelewa.Councillor Walladhu Muhaji : Kifungu cha kumi na moja Bwana Chairman, Haki za kifo: Maoni yangu ninapendelea nchiyetu ya Kenya kupatia usawa katika utumiyaji na kula matunda ya uhuru wetu, kwa wananchi wote. Kila wilaya wananchiwake halisi wafaidike na hayo mawili yanawezekana kupatikana.Ikiwa, kila kitu ikidaiwa na wananchi wenyewe, kwa hivyo napendekeza Serikali iwe ya Majimbo. Katika utawala wamajimbo lazima mkuu wa jimbo achaguliwe na raia. Wageni ambao si wananchi wasiwe na haki za kuchaguliwa au kuchagua.Na vile vile wageni wasiopatiwa uraia wakusajiliwa kwa karatasi wasiwe na uwezo wa kuchaguliwa kuwa viongozi wa wadhifawowote hata wa headmen au head-women.Com. Mosonik : Maliza---Councillor Walladhu Muhaji : Bwana Chairman namaliza. Nikifwatilisha kwa jimbo: lazima wafwasi wa dini mbali mbaliwatiliwe maanani katika Jimbo au majimbo ambayo Waislamu ni wengi sharia ya Islam lazima ifwatwe. Kwa sababu gani? Ilikukomesha ufisadi, wizi na maafa mengine. Mkubwa wa jimbo lazima awe Muislamu, au Makamu wake lazima awe Muislamu.Katika Jimbo au Majimbo wasiyo kuwa Waislamu, mtawala wa jimbo mkuu lazima awe Mkristu. Majimbo ndio mfumo wakipekee wenye kuleta maendeleo na mafanikio kwa wananchi. Lazima maafisa wote, watumishi wa uma, wawe wametokakatika wilaya hiyo: Kuanzia Wakuu wa wilaya, maafisa wa elimu, maafisa wa samaki, maafisa wa ukulima, ProvincialCommissioner, na ma-DOs, lazima watoke katika jimbo hilo hilo. Wananchi wenyewe kwa wenyewe sio kuletewa.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!