12.07.2015 Views

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS
  • No tags were found...

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

48Com. Mosonik: Councillor KichekoCouncillor Kicheko : Salaam Aleykum ..Kwanza nataka kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kuweza kutupatia nafasi kama hii kwa kuja kuchukua maoni kutoka kwawananchi wenyewe. Fursa kama hii mara nyingi hua siipati. Nashukuru Tume hii kwamba inaweza kufikiria kuchukua maonidirect kutoka kwa wananchi, halafu ipelekwe kwa Bunge ili iweze kutatuliwa. Nina imani kubwa ya kwamba katiba itawezakutengenezeka kwa haya ambayo tumezungumza.Kwanza, tunataka tuwe na serikali mbili. Ikiwa ni serikali ya majimbo. Pwani iwe na uongozi wake, na Bara nayo iwe nauongozi wake. Nikizungumza hivyo sisi hatutaweza kupata haki zetu, maana kwa siku nyingi huwa tumetawaliwa na serikalimoja lakini hatupati haki zetu, sisi watu wa Pwani. Rasilmali kubwa inatoka Pwani na haitekelezwi ipaswavyo kwa wananchiwaliozaliwa Pwani.Kwa hivyo ninaomba tuwe tunajivunia vitu vyetu vya pwani, na mtu wa pwani awe anaweza kuchaguliwa kuwa Rais. Lazimaawe raia wa Kenya, awe na umri usiyopungua miaka thelethini na tano, ateuliwe kwa chama cha kisiasa, ateulewe na watuwasiopungua elf moja kupitia kwa kura. Iwapo ni mtu mmoja tu awezaye kuchaguliwa, kisha mtu huyo ashinde kiti katikasehemu yake ya uchaguzi wa Bunge, katika uchaguzi mkuu, utangazwe kuwa Rais. Rais asiweze kuwa amiri mkuu wa majeshi.Mamlaka ni Bunge au kupitia kwa wananchi. Rais asiweze kuteuwa mawaziri, na manaibu, iwe ikipitia kwa Bunge. Raisasiweze kuteuwa mkuu wa sheria au wakuu wa Tume la uchaguzi au mahakimu, au ma-DC ambao (inaudible) za serikali.Mamlaka hayo ya kuteuwa mabalozi, Rais asipewe uwezo huo, ziwe zateuliwa na Wabunge.Makamu wa Rais: Ikiwa Rais amejiuuzulu au akiweza kupinduliwa,au akiwa mgonjwa au akiwa amekosa akili. Makamu waRais awe anatawala kwa muda wa siku sitini, na uweze kupiga kura baada ya mieze sita hivi, ndio kutateuliwa Rais. Iwapohakuna makamu wa Rais (inaudible), baraza la Mawaziri liteuwe waziri mmoja ashikilie.Serikali ya mitaa – Madiwani wawe watakuwa wamesoma kupungua angalau tayari darasa la saba, ili aweze kuhudumiawananchi wake vizuri. Ikiwezekana iende kwa kura ya maoni kwa wananchi wenyewe. Mayor awe akichaguliwa nawananchi, na Chairman awe vile vile akiteuliwa na wananchi, vipindi viwili kwa miaka miwili. Baadaye, anaweza kuteuliwa tenakwa muda wa miaka miwili. Ikiwa hatatekeleza wajibu wake, awe rahisi kutoka, na itapitia kwa kura ya wananchi. Halafu –councillors hao watalipwa ma Central government badala ya local government. Councillors wawe wanalipwa na Centralgovernment kama wale wabunge wanaolipwa na serikali. Pale kupitia kulipwa na serikali ya mitaa ndio wananchi inabidiwanyanyaswe kwa kufwata license, kwa mfano lete ndogo ndogo za kula ----- Kwa hivyo tunaomba councillors wawewatalipwa na Central government na (inaudible) ziwe zaenda kwa government.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!