12.07.2015 Views

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS
  • No tags were found...

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

26Kitu kingine napendekeza Katiba iunde ni kuhusu cheti cha kusafiri (Passport). Ningependekeza passport kwa wana<strong>kenya</strong>wote bila kuangalia kabila, rangi au dini. Ipeanwe kama kitambulisho. Imekuwa nitatizo sana kwa Waislamu kubaguliwakwenye kitu kama hiki.Sasa ningependa kupendekeza juu ya uchaguzi. Nikipendekeza Katiba ya uchaguzi unao kuja masanduku ya uchaguzi yaweyenye kuonyesha (yaani transparent). Hatutaki masanduku yenye giza hapa na kutuhadaa. Vile vile uchaguzi utakap<strong>of</strong>anyika,kura ihesabiwe kwa kila kituo. Wale ma-agent wanasimamia mambo ya kupigwa kura, wajue kile kituo kura ngapiziliandikishwa na ni kura ngapi zimepigwa, hatimaye wahesabu siku hiyo, hiyo, hapo, hapo. Mshindi wa uchaguzi ikiwa atakuwani councillor, au ni mbunge atangazwe kule ambapo atapata asili mia hamsini (50%) za kura zilizopigwa katika eneo lake. Simtu apewe kura mbili au kura moja awe kingoz,i hajakuwa kiongozi huyu. Kiongozi ni aliyepata kura asili mia hamsini (50%)na kura zote zilihesabiwa kama aanguke niza ubunge au za ucouncillor. Na ikiwa hawakufikia hivyo, basi mshindi wa kwanzana mshindi wa pili warudie round nyingine. Hapo hapo kwenye viongozi wa kisiasa, na hata viongozi wa kiutawala:ningependekeza Katiba itungwe kwamba mjumbe mbunge, councillor, hata chief na mfanyi kazi yeyote wa serikali lazima aweamefikia umri wa miaka 35. La si hivyo hajadhubutu kuwa kiongozi wa kisiasa.. Nilikuwa na mengi yu kuzungumza, lakinitulikuwa tukiomba hapo mbele ya kwamba tusirudie rudie ili tuweze. Sababu mengi ningetaka kusema wenzangu wameyasema.Kwa hayo machache nasema asante.Com. Mosonik : Ningependa kuuliza ni nini amesema, kuhusu nini? Umesema mwenzako amesema, lakini kuhusu nini?Shibala Mohamed: Yale yalikuwa ya kuzungumza ambayo wenzangu amezungumza ni juu ya wajibu wa Kadhi, kwa makamuna machief kadhi, mambo ya environment, yaani mali ya asili – natural resources, na mambo mengine ya wajumbe kuwa namajukumu ya kujinyakulia ile mishahara wanaotaka wao. Asante.Com. Mosonik : Swala lingine umesema kuhusu eneo ya waakilishi bungeni ama council, kwamba wawe na kura asili miahamsini (50%) na kuhusu Rais wa nchi?Shibala Mohamed: Hata hivyo Rais wa nchi vile vile mpaka apate asili mia hamsini (50%) za kura zote nchini. La, si hivyoarudiwe.Com. Mosonik : Nataka kuuliza tena, kama ulisoma kijitabu - - maswala na maswali, kuna swala letu: Je tuendelee kuwa nakanuni ya asili mia ishirini na tano (25%) ya waakilishi katika anga mikoa mitano, katika uchaguzi wa Rais au la?Shibala Mohamed: La, hatutaki hivyo. Tunataka Rais apate asili mia hamsini za kura zote nchini. Habari ya mikoa iondoke.Sababu mikoa inaenda kikabila. Kuna mikoa mingine, kuna makabila, kama Central, nitatoa mfano, ni Wakikuyu watupu.Kama Rift Valley nao ndivyo hivyo hivyo. Naweza kusema ni mbari moja - - Mkalenjini na Mnandi. Sababu ya kusema ni

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!