12.07.2015 Views

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS
  • No tags were found...

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

58pwani kwa karne nyingi zilizopita ziwezi hesabika. Waliomiliki ardhi za Lamu wakawa na mashamba, tukajenga manyumbaambayo kwamba hata watu kadha wanaokuja kututembelea ili kutuona wakaribishwa majumba hayo yaliojengwa wakati huo.Kwa hivyo, hivi ni kusema kuwa sisi ni wananchi wa Kenya wa kuzaliwa hapa nchini, bila shaka yoyote. Uraia wetu hauwezikutiliwa shaka na yeyote. Lakini wanaeleza masikitiko yao wakisema kuwa “tunashangazwa sana kuwa baada ya wazee wetukukaa kwa muda murefu na sisi kukaa kwa muda wote huo, kila unapomba vyeti vya kumiliki ardhi, huwa hatupewi.Wanasema, “tupendekeza ya kuwa: serikali itambue ardhi hiyo kwa milki yetu, kila mmoja apewe cheti cha kumiliki ardhi. Hakiitekelezwe kwa wote kwa sababu bila vyeti vya kumiliki ardhi, yaani Title Deeds, tunaweza kuzikosa hizo haki zetu.Sheria za kidini – Wasama maswala yote ya kuhusiana na dini ya Kislamu yamuliwe na Makadhi. Sheria ya mtu kuchaguliwakwa Kadhi ibadilishwe yaani mfumo ambao uko hivi sasa ubadilishwe. Wanasema.” Kadhi awe anachaguliwa: mtu mwenyeelimu ya dini ya kutosha, yaani awe mwanachuoni, awe sifa ya uaminivu, na mwendo mzuri kwa jumla. Sheria ya sasa yasisitizazaidi mtu awe amemaliza kidato cha nne, yaani Form four, na pengine hana elimu ya dini ya kutosha ya kuweza kutatuamaswala kama yale ya urathi, talaka na maswali mengineo muhimu. Pia wanasema,”iundwe kamati ya wanachuoni kutokapande zote ya Kenya, ili wafanye mahusiano kwa wale wanaopeleka maombi ya kuomba nafasi za Makadhi. Wanasemakuwa, “watakaopitishwa na wanavyuoni – yaani Masheikh, basi majina yao yakabidhiwe serikali, na watambue hao kama niMakadhi, waliochaguliwa na Masheikh wa Kislamu, bila ya kubadilishwa lugha hiyo. Kwa hivyo Rais awe hana uwezokabadilisha, isipokuwa afwatilia yale maagizo ya Masheikh walioamua. Wasema “serikali itambue Kadhi kuwa ni hakimu kamahakimu mwingine serikalini - - anapoamua kesi za Waislamu mtu asiwe na uwezo wa kwenda kupinga uamuzi huo katika kotinyingine yeyote, yaani tusiwe na uwezokano wa koti ya kuwa na appeal kwa mahakama nyingine isipokuwa za sheria zaKislamu.Elimu – Wanaeleza kuwa “elimu ya msingi kwote nchini itolewe bure, yaani free primary education. Wanaeleza kuwa “mzigowa karo za shule husababisha wazazi wengi kuwakatiza masomo watoto wao.Swala afya – Wanasema” kila tarafa kuwe na hospitali yenye vifaa vya kisasa na madakitari wa kutosha. Kwenda katikahospitali za wilaya yaani District hospitals, kutafuta matibabu ni jambo gumu. Wanaeleza kuwa, “kutafuta matibabu ni jambogumu, na shida za usafiri kulinganisha na mahali ambapo sisi tunaishi. Kwa hivyo wanapendekeza kwamba wagonjwawanapopelekwa mahospitalini kwa kuchukuliwa mbali kwa hospitali, na vile hospitali haiko karibu, kwa kuwa zilizopo hazinavifaa vya kutosha, basi wagonjwa wao pengine hufariki kabla hawajafika huko hospitalini. Kwa hivyo zile zahanati, yaani healthcentres ambazo ziko katika kila tarafa ziimarishwe.Swala la uchaguzi – Wanasema, “raia wanaopiga kura ya kuchagua Mbunge atakaye waakilisha Bungeni, wawe na uwezo wakupiga kura ya kutokuwa na imani na mbunge huyo iwapo hashugulikii masilahi yao. Kura ya kutokuwa na imani na mbungeipigwe miaka miwili baada ya kuchaguliwa kwa mbunge huyo. Wanapendekeza kuwa, “uchaguzi mdogo uitishwe kujaza nafasiya mbunge huyo, tuseme ambaye pengine amechaguliwa na hatamani tena kurudi kwao mpaka baada ya miaka mitano.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!