12.07.2015 Views

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS
  • No tags were found...

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

55suggestion kama hizo. Kwa hakika walisema huu mfumo wa 8-4.-4, ya eight years primary school, four years secondary or ‘O` Level and four years university, huwanyima nafasi. Kwa mfano kama ukitoka form four, watoto wengi hukaa nje, na tunajuakwamba serikali yetu ya Kenya hii sasa haiajiri watu. Hata tukifanya bidii tukienda ma-college watu wanatoka bila kazi. Lakinitukipata ile two years tukijiendelezha itakuwa ni nafasi kubwa kwa watu, badala ya kupotea na kwenda kufanya mamboambayo hayataki ka katika nchi, wawe wanaendelea na kusoma. Kwa sababu si rahisi, hivi sasa wanapomaliza masecondaryni wengi sana. Lakini wanavyopata nafasi ya kwenda chuo kikuu ni wachache sana. Lakini ikiweko two years shauri ya Alevel, itakuwa ni rahisi. Kwa sababu, ukikumbuka siku za nyuma, sehemu nyingi zilikuwa na high schools. Lakini sasa hakuna.Utaona ndio wasomi wengi wamekosa nafasi, na washerati, ufisadi na madhambi ya kila aina yanatokea. Kwa sababu wafwatamasomo na hakuna kazi. Wakiendelea na Form five na Form six, hatia zile zinapungua. Lakini kwa hapo mmefahamu vizuri.Com. Mosonik : Tausi Madinya,Speaker from the floor: Nafikiri ameenda.Com. Mosonik : Okay kuna councillor, no, Imam Hatma Suleiman na ufupishe tafadhali.Hatma Suleiman: Salaam Aleykum---------Mimi jina langu ni Hatma Suleiman wa Kizingitini hapo ni karibu ---.Mimi katika mambo yangu ni kwamba uchumi wetu wa Lamu Mashariki ni wa mikoko. Kwa hivyo twaomba mikoko ifunguliwenchini iwe atauzwa kwa mikoko hata ya nje, kama namna ilikuwa inatunzwa wakati wa Khayati Rais Kenyatta.Jambo la pili: sisi watu wa Lamu Mashariki hatuna umilikaji wa ardhi. Kwa hivyo tunaishi kama wageni. Tunataka tupatiweumilkaji wa ardhi kama wananchi wengine katika Kenya hii.Tatu: sisi watu wa Lamu Mashariki uchumi wetu ni wabahari. Kwa hivyo tunaomba kwamba kila kinachotokana na hii kiwekweruhusa ya kutumiwa kama sasa na kwa sababu ndio uchumi wetu sisi watu wa Pwani au sisi watu wa Lamu Mashariki. Vile vilesisi watu wa Lamu Mashariki tu watu bahari, tuingie sana bahari. Tunaomba kazi yote inayohusika bahari kama ya navy aukama ya kuzamia, tupatiwe sisi watu ambao kazi hiyo ndio kazi. Kama Wabara wakiwa ni watu kumi na wa pwani wawe kumikatika hilo jahazi au meli.Lingine: sisi Waislamu tunataka mambo yetu ya Kislamu iende kisheria ya kislamu bila ya kuguswa chochote yeyote aukupunguzwa chochote.Sisi watu wa Lamu Mashariki tunashida ya matibabu kwa ukosefu wa vifaa na madakitari wa juu na usafirishaji. Iwapokutatokea hatari kwa mgonjwa, kwa sababu ya uzazi au mengineo, tunashindwa. Huenda mtu yule atafariki, ilhali kwamba

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!