You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
MASWALI:

Al Akh Nusra: Sayyid tulikuwa na mushkil juu ya walimu na

mashekh wako wa kwanza walokusomesha.

Jawabu: Nilipelekwa chuoni kwa Sayyid Shekhe baba ake Sayyid

Hassan Shekh na alikuwa bibi msomeshaji mkubwa huko ni mwana Aisha,

wakimwita Mwana Ashati, nikisoma Qur an huko halafu baada ya kuhitimu

nikawa nasomesha huko huko chuoni. Mwisho nikaenda kwa chuo cha

Sayyied Abdul Fattah bin Ahmad ndugu yake Sayyid Abal Hassan nikawa

nasomesha huko na huko nilikuwa na wasaa mwingi kwa sababu niliachiwa

chuo jioni yote ningekuwa nayo mimi nikiendesha. Wakati huo huo kila

baina Magharib na Ishaa ninakwenda msikitini, nilimuogopa sana Shariff

Aboud, wa pili Sayyid Abdul Fattah alikuwa mkali. Siku moja sikwenda

Msikitini akanambia: “Baada ya leo ikiwa hukuja msikitini utaona”.

Tangu siku hiyo mpaka leo ikifika Magharib na Ishaa hutafuta pahali penye

Msikiti niingie kwa woga nilioupata kwa hiyo nilikwenda akanianzisha

Babu baada ya Babu nikasoma Safina halafu Risala halafu Taali-mul

mutaalim, Durarul bahia, Riadhal badia, Muqadimatu hadhramiya,

Rubul ibada, Ghaya. Nilipofika kwenye Babu swalatu mayyit, intakal

ila rahmati Lah na sikwenda kusoma kwa yeyote siku ambazo nnasoma huko

illa kwa Sayyied Abal Hassan nikisoma na Nahau siku alizokuwako Unguja,

kenda Pemba siku nyingi. Ikawa nakwenda kidogo kidogo sana kama

natambaa lakini Taalimul-mutaallim inasema usifanye ghasia kubadilisha

badilisha walimu kwa hivyo nimekaa vile vile ikiwa wale walimu

wanakutosheleza bila shaka lakini Mwalimu unamuona si mwalimu

wakutosheleza kwa kukuongoza ukitaka kwenda kwa mwengine akwambie

aa unaambiwa huna rukhsa, rukhsa, mtu hupata mwalimu wa kweli.

Halafu darasa akaichukuwa Sayyid Abal Hassan tukasoma

Umdatus salik Msikitini kwa Shariff Abudu Msikiti wa Vikokotoni pale

yote yanapita hapo. Kulikuwa Msikiti Vikokotoni pale tukisoma Umdatu

salik hivo hivyo tukawa tunasoma kidogo kidogo sana mara anasafiri

anakwenda Pemba akachume Karafuu, afanye basi hivyo hivyo, kidogo

kidogo. Tukaja tukaanza na shereh ya Ghaya baada tulipomaliza Umdati

salik ikawa wakati huo ikawa nakwenda Darasani kwa Sayyid bin Jafar.

Ikawa nasoma kidogo kidogo bila ya darasa Mimi mwenyewe tu kama

Bidaayatul hidayat katika vitabu nakumbuka nilisoma. Bidayatul hidaya

nilisoma na kitabu cha Mashairi Fiqhi Zubad na darasani kwake kila

asubuhi kila nikiwa sendi Skuli hapa skuli au nilipokuwa nipo

16.