Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
vyeo kama alivyokuwa Sayyidna Abdul Qadir “Mikh-daa”?

Jawabu: Wako waliofika huko, wako wasiofika, wako walofika wako

wasofika bila shaka Lahum Dara-ja-tun-indal Lah.

Swali (11) Al Akh Abdul Samad: Cheo cha Mikda Sayyidna Abdul

Qadir katunukiwa na nani?

Jawabu: Kajitahidi kafanya mujahada kapigana na Nafsi kaenda kazunguka

katika majangwa miaka na miaka na miaka kaivunja Nafsi yake kaivunja kabisa

hata hamna kitu. Hivyo ndio njia ya kupatia Uwalii, kuivunja Nafsi hata katika

alama ya kuwa kaivunja Nafsi yake kabisa aliazimia kufunga miaka 15

mfululizo. Siku ya mwisho ya kufunga miaka kumi na tano karibu na magharibi

akamuona mtu - Rehmal Lahu man shariba ha-dhal ma-l. “Mwenyezi

Mungu amrehemu mtu atakaekunywa maji haya” Sayyidna Abdul Qadir

akasema “Nini funga yangu ya miaka 15 mbele ya dua ya mtu huyu”.

Na hajapata kukutana nae lakini Nafsi yake ilivunjika Tawa-dhui isokuwa na

kiasi Mungu akamnyanyua cheo kikubwa. Seyyidna Ahmad Rifa-i katika

yalomnyanyua sana kulikuwa na mbwa mgonjwa na Seyyidna Ahmad Rifai

bado madhehebu yake ni Shafii na Mbwa ni najisi Mughalladha kwa Shafii

akamchukuwa akaenda nje ya mji akamkogesha akampa dawa na nini mpaka

akapona Mwenyezi Mungu akapendezewa nae khasir Nufus.

Swali (12) Akh. Abdul Samad: Katika ubeti wa Manaqib wa Seyyidna

Abdul Qadir: “Wakulu Walii lahu Qadami waana Qadami Nabii badiri

tamami…….”

Jawabu: Haya baada ya kwisha huko juu.

Swali (13) Akh. Abdul Samad; Basi amemkanyaga vipi Mtume SAW

kwenye Unyayo?

Jawabu: Walii, Walii, hakusema Nabii. Qadami ala raqbatil kuli Walii.

Lakini wanasema Mawalii wengi kuwa hii sio iliomtafautisha Sayyidna Abdul

Qadir na Mawalii wengine alikuwa juu sana kuliko hapa wako Mawalii wengine

wanapata Daraja hiyo hata wanawake hii ni daraja tu Maqama basi Sayyidna

Abdul Qadir yuko wapi na Mambo yalomtafautisha na Mawaliii wengine.

Swali (14) Akh. Abdul Samad: Ni sahihi katika kisa cha miraji

26.