You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
DIBAJI

Al – hamdul-lillah wa swalatu was salaam alaa Khayru Khalqillah Sayyidna

Muhammad wa A-lihi wa Swahbihi waman waala wa Baad.

Hichi ni kitabu ambacho Al- habib Sayyid Omar Bin Abdallah mashuhuri

kwa jina Mwinyi-Baraka katika wajukuu wa Sayyid Abu-bakkar Bin Salim-Mola

Enaat huko Hadharamut, kwa taabu alielezea mwenyewe akiwa amejinyoosha

kwenye kitanda alipokua mgeni wa Bw. Mohamed Khan Shemeji yake na Al- marhum

Swaahib El - Ishara Bw. Akram Mohd aliyefia Mwanza kati ya Mwaka 1988 na

89 Mwanza-Tanzania Allahu Yarhamuhu wa Jamill Muuminina Wal Muuminaat.

Alikua akizungumza kwa shida sana pengine Dak. 10. Pengine ndo gha-ya

Dak. 15. Kwa hiyo ilikuwa tukimfwata na Tepu Recorder mara kwa mara tukiwa na

Akh. Aly Mzee Comorian toka Mkunguni kwa Al-marhumu Mohamed Bin Mahdi na

wanawe kina Akh. Islam, Khamis na Al-marhumu Mahdy Mohamed Mahdy

Allahummaghfir-lahum wa yarhamhum jamiia.

Al-hamdu-lillah tuliwahi kumaliza kunasa na kunukuru yote kuhusu safari

zake za Europe na Amerika kama itavoonekana ndani yake. Kwa vile lengo kubwa

la safari zake tukiacha kusoma ilikua ni Jihadi katika Dini ya Mnyezi Mungu nayo si

nyingine bali ni Uislamu, tumeonelea kukiita “Mwinyi Baraka katika Ulimwengu

wa Uislamu” tukitegemea kwa imani zote kua:

(a)

(b)

(c)

kitazagaza maarifa mazuri kwa watakaokisoma.

kutakua angalau na kumbukumbu ya mmoja wa wanafalsafa wa

Kisufi mkubwa lakini hakupata umashuhuri nchini kwao mpaka

amekufa.

Tutafaulu Insha-allah kumjulisha yule ambae hakumjua

mwanachuoni mkubwa huyo wa East -Africa na labda kumuigiza

au kumtakia dua, kwani ipo hasara kubwa kwa kule kushindwa

kumtumia vile ambavyo ingepasa.

Tabia yake katika kujitupa chini na kujiona kua si kitu alifahamika vibaya

kwa ambao hawakumjua, na hijabu ya wazi wazi kwa walomjua vizuri kabisa. Dalili

kubwa ilionekana mara nyingi alipokuwepo Jijini hapa, si wengi walojua, kwa hiyo

ilifikia mpaka anaondoka si wengi walokua na habari hata ile ya kuepo Jijini hadi

kufikia mwezi mzima! mara kadhaa alipata mwaliko kwa mwanafunzi wake

mkubwa, alipokua madarakani

vi.