Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
MASWALI:

Swali (1) Al Akh. Sabri: Nafsi inakaa katika Roho au Moyo?

Jawabu: Ndo wewe Nafsi, Nafsi ndo wewe.

Swali (2) Al Akh. Sabri: Nataka kuelewa makaazi yeke ni

wapi?

Jawabu: Haina makaazi ndo wewe. Si wewe umeazimia kuja hapa leo? Basi

wewe ndio Nafsi, haina pahala mahsusi na Roho ndo Nafsi yenyewe lakini

inapokwenda juu sana ikatakasika ikasafika ikatulizana inaitwa Roho. Na Roho

ina maana hicho kinachotupa uhai. Ina maana kadha wa kadha. Ukitafuta

Roho katika mwili huiyoni na Moyo kazi yake nyengine. na Moyo wanautumia

Sufia kwa maana mbili tatu. Moyo huu kama wakinga kinga na wa mwengineo

na Bin Adam wake anayo hiyo hiyo- Saalal lahul afwal-afya-kuna na Moyo

wanautumia hiyo Nafsi inapogeuka ikinyanyuka hali fulani wanaita Qalbi lakini

hayo ndio hayo nnochotaka kuja kusema: “Nafsi ndio wewe”.

Swali (3) Al Akh Marjebi: Nauliza kwamba hii nafsi inapobadilika

kutoka katika Nafsil Ammaral, Nafsi Lawamma Nafsil Mulhima inakuwa

ile Nafsi yenyewe au mwili unabadilika?

Jawabu: Ni Nafsi. Mwili haubadiliki kitu mwili unakuwa controlled na zile

Nafsi ikiwa Al Ammara, unayoipeleka katika mchezo ikiwa Lawwama

unaipeleka huko mwili hauna kazi mwili na kama dubwana la mutukari lile basi

ukipeleka speed kubwa ikipeleka ndogo ukipeleka huku unafaata basi

unategemea uko katika hali gani.

Swali (4)Al Akh Abdul Samad: Na kila Nafsi kutoka katika ile ya

mwanzo mpaka hiyo ya mwisho kuna nyuradi maalumu ambazo unaweza

ukafanya ziweze kubadilika?

Jawabu: Naam, ukipata mlezi kama hapana walezi unapochukuwa kidogo

unatoka katika hali moja katika hali ya pili iliyobaki ni kukithiri nyuradi

unazopewa za Twariqa zinafanya sababu hata unageuka kutoka kwenye hali moja

na kwenda kwenye hali nyengine mwanzo mwanzo hapana kama kuleta Lailaha-illaa

Llahu mara nyingi kila ukiweza, njiani wapi wapi La ilaha illa

Llahu ndio dawa ya watu kama sisi wenye Nafsir Ammarat bi sui mpaka

atakapokwenda mbele.

23.