Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
nilipokuweko hapo hapana mtu alosalisha isipokuwa mimi. Basi kwa

hivyo wengi hawa Makhalifa wa Twariqal Qadiriya, furui kadha wa

kadha nimekutana nao. Furui zipo nyingi za Twariqatil Qadiriya na

katika hao ni Sayyid Ashekh Muhammed el fa-tih- ndo alotupenda

sana Sudan, wala si mtu mzee sana . Allah yamunnu alayhi bil a-

fiya.

Wao silsila yao Branch yao ni As-sammaa-ni na huyo

As-sammaa-ni alikuweko Ijaz babu yake ndo alochukuwa huko na

Baba yake akaja akawa Khalifa Walii Mkubwa halafu akaja akachukua

yeye.

Nikakutana na mwengine Khano khalafu ndo nimekuja nikajua

kuwa yeye kachukuwa Twariqa kwa huyo Bwana Muhammed El

Fatah khalafu kenda Baghdad kenda kukamilisha.

Vile vile nimekutana na Khano mtu wa ajabu, mtu wa ajabu

mwana chuoni mlezi ana watu kadha wa kadha anawalea na anavitabu

katunga na hivi natawadhui kubwa nilipokwenda kumtizama kakataa

kukaa juu ya kiti nikamwambia basi na mie sikai nikamwambia basi

kama hukai nitamwambia mtoto akalete kiti: “Mtoto lete kiti”,

kumbe halafu kamuashiria kua usilete kenda kakaa chini Ah! Mie

nangojea kiti hapa mpaka tumeondoka kiti hakijaja. Tukaja

tukakutana na Muridi wengi wengine watu wa Biashara wakubwa watu

wa nini watu namna kwa namna.

Siku moja nimekutana nae katika Baytullahil Hara-m, hata

akanambia kuwa kenda Baghdadi kaambiwa kule Baghdadi kua “Kaja

Umar Abdallah hapa” na Mashekhe wetu wa huku kama Sayyid Abal

Hassan na wengineo na nimekutana nao Pakistani, Siria, Masri,

Maghrib wapi, wapi wamejaa Masheikhe wa Al Qadiriya ndo maana

nikasema: “Aja-zani ghayra wa-hidin fi Twariqatil Qadiriyya”

Wa awwal man ad-khalani fi ha-dhihi da-ira mwanzo

alonitia ndani ya daira hii, Huwa Seyyid Swa-fis sarira- ndani ya

Roho yake ni safi Alladhi kana lahu an twawri Nafsihi mayyil.

Hamili upande wa Nafsi, Abdul Fat-tah bin Ahmad Jamali Leyl

huyu ndugu yake mkubwa Sayyid Abal Hassan Mkubwa wake ndo

mwanzo tangu udogoni alinichukuwa tunakwenda kwenye daira

32.