You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Swali la nne: Ungetufafanulia vipi kuhusu Twarika (kinjia ya)

Dhwahir na batwin, na nini hukumu ya mwenye kupinga kufaa kwake

(katika Uislamu kwa Jumla)?

Jawabu: Hiyo peke yake sio mambo madogo ukisema kidogo utapoteza

watu

Swali la tano: Ungetufafanulia vipi kuhusu swala la Mahaba kwa

jumla na kuna tafauti gani kati yake na Ishq na

Ishtiyaq na Wudd.

Jawabu: Hilo ndo kabisa halisemeki haiwi kabisa, hayasemeki

Swali la sita: Nini ufananuzi wa hizi nafsi saba (1) Al ammarat (2) Al

lawama (3) Al Mulhima (4) Al Mutmaina (5) Al Radhiya (6) Al Mardhia

(7)Al Kamila?

Jawabu: Wama-ubarriu nafsi-inna nafsa ha ammaratu bi sui…………….. Hilo

kadhalika nilijaribu karibu karibuni nimeanza kushika Msikiti Jibril Al khamis

baada ya kusomwa Ratibul Attas, tukiwapo Unguja. Siku moja nimesoma

Nafsil ammara na sikumaliza kwa hivyo itachukua muda hata mtu azimalize

nafsi hizo. Na ni maneno yenye faida sana kwa watu namna kwa namna hata

wasiokuwa Waislamu. Nakumbuka nilikwenda Makerere niliitwa kutoa

khutba moja juu yake sijui niliita nini lakini nilipita njia hiyo walikuwa

Amerikans nani na nani. Wakastaajabu sana. Nilikuwa safari moja. Nilikuwa

Malay siku zile ilikuwa Maley kabla haijaja Malaysia. Nikenda pahala

nikachukuliwa pahala nikenda nikatoa khutuba nikaalikwa nikaambiwa

Jumaatano wanakusanyika watu wa Dini namna kwa namna, na kila wiki anatoa

mmoja katika mtu wa dini moja wapo (na siku ile ilikuwa zamu ya dini ya

mkiristo) lakini kwa wewe tulivyokusikia leo unasema tutakupa fursa wewe

useme. Nilikuwa katika nyumba ya Ambasidor baada ya kutoa khutba yule

Ambasidor akaniambia: “Ahsante sana, Today for the first time I have

Understood may religion” anasema leo kwa mara ya mwanzo nimeifahamu

dini yangu mwenyewe lakini nilikuwa hata sifahamu, lakini leo ndio kwanza

nimefahamu kupitia njia hizi- Al Ammara, Lawama, Mulhima, Mutmaina,

Radhia, Mardhia, kamila. Jazaka llahu kheir. Mara nyingi nimepita njia hiyo

kila pahala. Kidogo pana migeuzo geuzo kidogo lakini ni msingi mkubwa wa

spiritualism. Spritual Development.

Wafaqana Llahu lima yuhibu wa yardha.

18.