Kutetea Haki za Binadamu - East and Horn of Africa Human Rights ...
Kutetea Haki za Binadamu - East and Horn of Africa Human Rights ...
Kutetea Haki za Binadamu - East and Horn of Africa Human Rights ...
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
mengine, iwapo mtetezi anakuwa mlengwa au la

hutegemea matokeo ya kazi yao kwa watendaji wa

kutumia silaha.

Uwezekano wa kudhurika (kiwango ambacho

watetezi ni rahisi kukabiliwa na hasara, uharibifu,

mateso, na kifo, katika tukio la mashambulizi)

hutofautiana kwa kila mtetezi au shirika lisilo la

kiserikali, na pia hutofautiana kutokana na muda.

Uwezekano wa kudhurika ni kipimo husika, kwa

kuwa watu wote na makundi yote yana uwezekano

wa kudhurika, lakini kila moja, kulingana na

mazingira na hali zao na hili lina kiwango na aina

yake lenyewe ya uwezekano wa kudhurika. Kwa

mfano, mtetezi wa haki za binadamu ana uwezekano

zaidi wa kudhurika anapokuwa nje, barabarani kuliko

anapokuwa ofisini kwake (iwapo imelindwa vizuri).

Uwezekano wa kudhurika kwa shirika lisilo la

kiserikali linaweza kuonekana kuathirika kwa

sababu mbalimbali, kama vile kuachwa wazi

(kiwango ambacho mfanyakazi na mali ya shirika

lisilo la kiserikali inakuwa katika mahali hatari au

pasipolindwa), athari ya mpango wa kazi (ikiwa

kazi ya shirika lisilo la kiserikali ina athari mbaya

kwa mtendaji yeyote anayetumia silaha, huliweka

shirika hilo lisilo la kiserikali katika uwezekano wa

kudhurika) n.k. 7

Uwezo ni nguvu na rasilimali zilizopo kwa kundi

au mtu binafsi ili kufikia kiwango cha kuridhisha

cha usalama (au heshima kwa haki zao/zake za

binadamu). Mifano ya uwezo ni mafunzo (katika

usalama, katika masuala ya kisheria, nk), kazi ya

kikundi kama timu, nk.

Hatari iliyosababishwa na tishio na uwezekano wa

kudhurika vinaweza kupungua ikiwa watetezi wana

uwezo wa kutosha (kadri kunapokuwa na uwezo

zaidi, ndivyo kadri hatari inavyopungua):

Hatari = vitisho x uwezekano wa kudhurika

uwezo

Kwa kuweka muhtasari wa aya zilizotangulia katika

kielelezo tunachofanyia kazi, ili kupunguza hatari

kwa viwango vinavyokubalika inabidi:

• Kupunguza vitisho

• Kupunguza/kuboresha mambo yanayofanya

uwezekano wa kudhurika

7 Kikomo muhimu cha urefu wa makala hii kinatufanya tusiingize

kielelezo chenye maelezo ya kina kuhusu aina na kazi ya

sababu kuu za uwezekano wa kudhurika.

• Kuongeza uwezo wa usalama kwa mafunzo ya

usalama katika usalama, tathmini ya hatari nk

Kulenga

• Uchambuzi wa hali

• Tathmini ya vitisho

HATARI =

Kupunguza

uwezekano wa

kudhurika

VITISHO X UWEZEKANO

WA KUDHURUKA

UWEZO

Kuimarisha/kukuza

uwezo

Lazima tuzingatie kuwa hatari ni dhana inayobadilika

na hubadilika kulingana na wakati, ikifuata mabadiliko

katika vitisho, uwezekano wa kudhurika na

uwezo. Inafanya haja ya kutathmini hatari mara kwa

mara, na hasa ikiwa kuna mabadiliko katika mazingira

ya kazi, katika vitisho au katika uwezekano

wa kudhurika. Kwa mfano, hatari huongezeka zaidi

mtendaji anapojisikia kuzungukwa; uwezekano wa

kudhurika huongezeka mfanyakazi mpya wa kutumia

silaha anapoanza kufanya kazi bila mafunzo stahiki.

Hatua za usalama kama kamera ya video au

gari lenye kinga zinaweza kupunguza hatari kwa

kuyavunja nguvu mambo yanayoleta uwezekano wa

kudhurika, lakini hatua hizo hazikabiliani na chanzo

kikuu cha hatari, ambacho hutokana na vitisho na

shauku ya kuzitumia, ikiwa hatua dhidi ya watetezi

hazitolewi adhabu. Kwa sababu hizi, hatua zote

kubwa katika ulinzi zinapaswa zilenge kupunguza

vitisho hivyo, pamoja na mambo yanayopunguza

uwezekano wa kudhurika.

Kupanga mipango ya kazi na usalama

Usimamizi wa usalama lazima uingizwe katika kila

hatua iliyofanyiwa uchambuzi wakati wa kuunda

mpango wa kazi.

Usalama una pembe maalum unapofanya

uchambuzi wa mazingira na kuweka malengo na

madhumuni ya kazi, vile vile wakati wa kuunda

mpango wa kazi, kufuatilia na kutathmini matokeo

yake. Miongozo ya usalama ina mahali maalum

(katika hatua ya kupanga) katika mchakato mzima,

ambapo zinakuwa nyaraka hai ambazo hupata

Kutetea Haki za Binadamu: Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu | Toleo la pili 13