Kutetea Haki za Binadamu - East and Horn of Africa Human Rights ...
Kutetea Haki za Binadamu - East and Horn of Africa Human Rights ...
Kutetea Haki za Binadamu - East and Horn of Africa Human Rights ...
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Sura ya 4

Kampeni za Utetezi wa Haki za Binadamu

Mikakati ya kuendesha kampeni, kushawishi, na

kazi ya utetezi vinaweza kutumika kama zana na

watetezi wa haki za binadamu katika kazi yao ya

kulinda haki za watu wengine. Malengo ya kufanya

kampeni ni kuleta mabadiliko chanya, kuwafanya

watu watekeleze dhamira zao au kutimiza wajibu na

majukumu yao. Pia zinaweza kutumika katika kukuza

uelewa wa masuala fulani kwa mapana. Makala hii

inataka kutoa maelezo ya jumla ya msingi juu ya

namna ya kubuni mikakati ya kampeni inayofaa kwa

masuala mbalimbali na asili 19 tofauti za mashirika.

Kufanya kampeni juu ya haki za binadamu ni

njia muhimu ya kutafuta ukiukwaji wa haki za

binadamu na kuwafidia wale ambao haki zao

zimekiukwa. Watu binafsi na jamii wanaweza

kutetea haki zao wenyewe (angalia ukuaji wa hivi

karibuni wa uhamasishaji wa raia) au wengine

wanaweza kufanya kampeni kwa niaba yao, hasa

pale ambapo makundi hayana ufahamu wa haki zao

wenyewe au ushawishi wa kudai mabadiliko. Kwa

mujibu wa Kifungu cha 1 cha Azimio la Umoja wa

Mataifa kuhusu Watetezi 20 wa Haki za Binadamu,

“Kila mmoja ana haki, mtu mmoja mmoja na kwa

kushirikiana na wengine, kukuza na kujitahidi kwa

ajili ya ulinzi na utekelezaji wa haki za binadamu na

uhuru wa msingi katika ngazi za mkoa, taifa na ya

kimataifa”. Kwa kweli, kila mtu ana haki ya kufanya

kampeni kwa ajili ya haki za wengine pia na zao

wenyewe.

Mipango ya kampeni

Ili kampeni iwe ya mafanikio, lazima malengo

yawekwe kutegemea na mabadiliko unayotaka

kuleta. Malengo haya ni lazima yawe maalum,

yanayopimika, yanayotekelezeka, yenye uhalisia na

wakati maalum. Ili kujua malengo yako ni maalum

au yanapimika namna gani, lazima kwanza ujiulize

kile wewe mwenyewe unachotumaini na kutarajia

kuwa kitakuwa tofauti baada ya kampeni.

19 Makala halisi ya Carol Magambo na kufanyiwa marekebisho

na Rachel Nicholson Kiambatanishi cha vyombo vya habari

vya Kijamii (Sura ya 4.5) na Neil Blazevic

20 Jina kamili la Azimio ni: Azimio kuhusu Haki na Majukumu ya

Watu binafsi, Makundi na Vyombo Vya Kijamii Kuendeleza na

Kulinda Kiulimwengu Haki za Binadamu Zinazotambuliwa

na Uhuru wa Msingi. Inaweza kupatikana kupitia Ofisi ya

Ubalozi wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu: http://

www.ohchr.org/english/law/freedom.htm

Pili, inabidi ufanyike utafiti ili kupata taarifa kwa ajili

ya mkakati wa kampeni yako. Kuelewa kikamilifu

masuala yaliyo hatarini ndiko kutakakosaidia uundaji

wa mkakati madhubuti. Hii itakusaidia kufafanua

tatizo unalojaribu kutatua na kufahamu, kwa mfano,

nani hukiuka na kwa nini haya hutokea. Unapofanya

utafiti ni lazima pia uweze kujibu maswali kama vile

ni ujumbe gani tunaojaribu kutoa na ni mabadiliko

gani tunayotaka kuyapata Kwa nini tunataka

mabadiliko haya Tunamlenga nani – ni wadau na

wabeba jukumu gani walio na ushawishi juu ya suala

hili Tulifanye namna gani jambo hili na tutumie

njia ipi Je, ni kwa njia ya intaneti, simu, vyombo

vya habari, mihadhara, mijadala, maandamano,

maonyesho au maandalizi ya dua Juhudi zetu

tuzilenge wapi Je, ni katika ngazi ya mahali husika,

kitaifa, kikanda au kimataifa Na mwisho kampeni

hiyo itafanyika lini Mtu anapofanya utafiti juu

ya masuala ya kampeni, inabidi aunde njia bora

ya kufikia malengo na kutumia mchanganyiko wa

mbinu mbalimbali za kampeni ambazo tutaziangalia

baadaye. Majadiliano ya timu ya kampeni juu ya

mbinu za kutumia yatathibitika kuwa ya manufaa

kwani itabidi faida na hasara zake zipimwe.

Huu ni mfano wa kampeni maalum, inayokwenda

hatua kwa hatua kupitia utafiti na mchakato wa

mpango:

Wewe ni shirika la kijamii la kiraia nchini Uganda

ambaye unataka kuona Muswada wa Sheria ya

Mahusiano ya Nchini unapitishwa. Inabidi ujiulize,

kwa nini tunahitaji Muswada huu upitishwe

Kutoa usawa kwa wanawake na wanaume katika

mambo yanayohusiana na ndoa, talaka na mali ya

familia.

Kwa nini mpaka sasa haijapitishwa

Kutokana na upinzani toka idara fulani za jamii.

Watu gani wana ushawishi katika mukhtadha huu

Wabunge, Mawaziri na wafanyakazi wa Wizara ya

Jinsia.

Sawa, kwa hiyo tutawashawishije watekeleze

Je, hilo linaweza kufanywa kwa kutia sahihi maombi,

maandamano au mikutano ya hadhara, au utetezi

binafsi kwa njia ya barua na mikutano itafaa zaidi

Nani mwingine anafanyia kazi suala hili – tunaweza

kuunda mitandao na mashirika mengine ya vyama

28

Kutetea Haki za Binadamu: Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu | Toleo la pili