16.01.2015 Views

Kutetea Haki za Binadamu - East and Horn of Africa Human Rights ...

Kutetea Haki za Binadamu - East and Horn of Africa Human Rights ...

Kutetea Haki za Binadamu - East and Horn of Africa Human Rights ...

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

na kimwili peke yake haitoshi kwa kushughulikia

athari za kiwewe na maelezo ya vurugu inabidi

yachukuliwe kama suala tofauti ili kukuza ufahamu

wa upana wa madhara yake na njia inayofaa

kushughulikia suala hili.

Katika juhudi za kushughulikia mahitaji ya

wanusurikaji wa vurugu wakati wa mapambano

na mateso yaliyofanywa dhidi ya watu binafsi,

familia na jamii, Kituo cha Kanada kwa Wahanga

wa Mateso hutumia dhana ya kiwewe na madhara

ya kisaikolojia kama ilivyofafanuliwa na Ignacio

Martin-Baro. Martin-Baro alikuwa Kasisi wa

Wajesuti wa Kihispania na mwanasaikolojia

aliyefanya kazi El Salvador katika miaka ya 1980.

Kazi yake imekuwa ikichapishwa na Chuo Kikuu

cha Harvard. Alipofuatwa na wenzake wa Harvard

waliotaka kutafsiri kazi yake, alijibu: “Katika dunia

yako, ni kuchapisha au kuangamia. Katika yangu,

ni kuchapisha na kuangamia.” Na hakika, aliuawa

mwaka 1989 na kikosi cha mauaji huko El Salvador

katika mauaji ya watu wengi na mtunza nyumba

wake, binti yake na makasisi na wasomi wengine

kadhaa wakifanya kazi ugani.

Nadharia yake ilielezea jinsi “tabia za kiwewe”

zinavyojitokeza. Dhana hii inatoa pia utaratibu

ambao Kituo cha Kanada kwa Wahanga wa Mateso

hutekelezea mtindo wake wa utoaji huduma kwa

wanusurikaji wa mateso. Ni mtindo wa jumla

ambao huchanganya huduma ili kukidhi mahitaji ya

wanusurikaji wa mateso. Inahusisha huduma “katika

ofisi ya shirika” na mtandao mkubwa (mpana) wa

watu binafsi na mashirika ambayo hutoa huduma

kwa wateja wa Kituo cha Kanada kwa Waathirika wa

Mateso au huwaunganisha na mitandao mingine

ambapo mahitaji yao yanaweza kutimizwa.

Kwa mujibu wa Martin-Baro, kuna vipengele vitatu

vya kiwewe cha kisaikolojia:

1. Wakati mtu hubaki kuwa mhanga mkuu

wa vurugu za kupangwa, aina ya kiwewe

hutegemea vyanzo vyake kijamii.

Mateso na vurugu za kupangwa kimsingi ni

matatizo ya kijamii, na si matendo ya tahadhari

ya watu binafsi. Hutokea kama njia ya udhibiti

wa kijamii na kwa kuwa idhini imetolewa

kwa ngazi nyingi. Mhalifu amepewa idhini

na msimamizi wake wa karibu, msimamizi

na kamanda wake, na kuendelea hivyo hadi

madaraka ya juu zaidi. Jamii inaweza pia

kushiriki katika hili kwa njia ya ukimya wao na

kukana kutokea kwa matendo haya.

2. Kwa kuwa kiwewe hujengwa kijamii, mhanga

binafsi hali kadhalika na sababu za kijamii

zinazochochea zinahitaji tiba na ufumbuzi.

Haitoshi kumfunga mtu bendeji. Ikiwa

atapelekwa tena katika mazingira hayo hayo

ambayo yanasababisha kiwewe kutokea, basi

atatiwa kiwewe tena. Iwapo mateso na vurugu

za kupangwa ni tatizo la kijamii, basi ufumbuzi

wake lazima pia uwe wa kijamii.

3. Kiwewe kitakuwa sugu iwapo mambo

yaliyosababisha kutokea kwake

hayajashughulikiwa hata kidogo.

Kiwewe cha kisaikolojia ni pamoja na kuelewa kuwa

vurugu za kupangwa hujenga mazingira ya “tabia za

kiwewe” kushamiri, wakati kukiwa na:

• Mgawanyiko wa kijamii na hakuna usawa;

• Kashfa za taasisi na maduru ya ukimya

vinagubika ukweli wa kijamii;

• Vurugu za kupangwa na vita vinaleta madhara

kwa watu binafsi na familia zao na mitandao

binafsi, pia jamii ambazo wao ni wahusika.

Unyimi ndio mfumo mkuu wa ulinzi unaotumiwa na

mtu binafsi, familia na jamii nzima. Inafanya kazi kwa

njia ifuatayo, kujenga kile Martin-Baro alichokiita

maduru ya ukimya:

Katika ngazi ya mtu binafsi mnusurikaji:

• Hudhibiti matukio - hataki kukumbuka.

• Anataka kuwalinda wengine kutokana na tukio

hilo lenye uchungu - hataki wengine wapatikane

na ubaya wa tukio hili.

• Hategemei kuelewa au kuaminika - wakati

mwingine huwa vigumu kuelewa jinsi watu

wanavyoweza kufanyiana ukatili, na mara nyingi,

hadithi za mateso zinaweza kuwa za ajabu

na zisizosadikika. Hii mara nyingi hufanywa

makusudi kabisa kwa upande wa wahalifu -

kufanya jambo la kutisha mno kiasi kwamba

kuliongelea kutachochea kutoamini. Pia, katika

tamaduni nyingine, kuna miiko mikali dhidi ya

kuzungumzia uzoefu fulani, hasa yanayohusu

ujinsia na ukatili wa kijinsia. Ni kawaida kwa

wahanga kulaumiwa kwa kile kilichowatokea

na wakati mwingine kufukuzwa nchini au

kupelekwa katika mauaji ya heshima.

• Hataki kumpa mtesaji nguvu kwa kuruhusu

matokeo ya kiwewe - ni vigumu kukubali

kuwa kupata kiwewe kungeweza kusababisha

madhara ambayo hayatibiki. Pia ni mfumo wa

kujihami unaofanya watu wafuate mtindo wa

maisha ya kawaida, lakini kwa kweli kwa kufanya

kazi kwa mateso.

Kutetea Haki za Binadamu: Kitabu cha Marejeo kwa watetezi wa Haki za Binadamu | Toleo la pili 21

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!