ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
134

yako, na ulianza kukatwa wakati tu uliajiriwa kazi. Sasa mpaka ufe tena ndio uje upewe hiyo pesa si unaona si vizuri Pengine

hata watoto wanaweza kufikiria kukuua ndio waje wachukuwe hio pesa yako. Afadhali upewe hizo pesa, ndio uangalie welfare

ya watoto wako ukiwa hai.

Com. Ratanya: Sasa unataka review ya hiyo part ya Act hiyo ya pension

Morris Gichaga: Ndio. Ya pili, sijaandika hiyo, hiyo nimeandika ni hiyo nimetaja, ya pili, ni katika vile tunaishi huku kwetu

mashambani huku.

Security – tunaambiwa mara kwa mara, hati wale watu wako na buduki zao, ambazo hawakuchukua kwa hari ya kawaida

warudishe kwa serikali, ukirudisha, zingine unasikia zimetokea upande huyu mwingine, unakuja unapigwa unanyang’anywa mali

yako, kama ni ng’ombe zinaenda, wanakuja wanachoma hata nyumba zako, sababu unaogopa kupigana na hao sababu wako

na buduki. Sasa serikali haitilii maanane sana wakati unarudisha buduki, wahakikishe kila mtu amerudisha ndio watulinde, lakini

wanarudisha upande mmoja na mwingine unambaki sasa kupigwa. Sasa, kama wanaona wanashidwa kututisha hizo buduki

zote, waturuhusu kila nyumba ama tuseme kila village ipewe walinzi kwa sababu hata ukienda kwa chief ama kwa wapi,

unaambiwa buduki hakuna hapa. Ata chief anajificha kwa msitu wakati wewe unaenda kujificha. Sasa kama ingewezekana, kila

village, ipewe, wazee kama wawili watatu hivi wawe na buduki ya halali kutoka kwa serikali, walinde mali yao kwa sababu hata

ukitegemea serikali sasa mali yako inaisha na hakuna mtu anakusaidia. Ni hayo tu nilikuwa nayo Bwana Commissioner. Asante

sana.

Com. Ratanya: Asante sana Morris kwa hayo machache yako, twende kwa Genevasi.

Genevasi Kubai: Nasema asante, mimi naitwa Genevasi Kubai, maoni yangu ni juu ya ukulima. Tunataka serikali, iangalie

wakulima kwa sababu saa ingine tunalima kahawa, tukipeleka huko factory, wakati pesa inakuja tunaambiwa hakuna pesa,

kahawa yenu iliharibika. Saa ingine tukaambiwa mlilipwa pay out. Sasa wakulima sisi tunaumizwa, hatujui tutafanya kazi ingine

wapi kwa sababu ukulima, serikali haituangalii kwenye ukulima, tunataka serikali ituangalie tukiwa wakulima. Ndio mimi

nasema.

Com. Ratanya: Okey asante sana, tumeshukuru, twende kwa Christine Muthau,

Christine Muthau: Jina langu ni naitwa Christine Muthau, (then speaks in vernacular)

Com. Ratanya: Uga riatwa riaku kiri microphone muthee wakwa .

Utaje jina kwenya microphone mzee wangu,

Peter N’toitharia: Naitwa Peter N’toitharia, jambo la kwanza nataka kuongea mambo ya Rais, mimi ningependelea, Rais