05.01.2015 Views

ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet

ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet

ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

59

wajumbe wake. Ningependelea vile vile President asiwe ni Member of Parliament ili aweze kuwa an control constituencies zote

za Kenya bila kupendelea constituency moja ambayo anasema ni yake. Ikiwa hivyo President atakuwa ni mjumbe wa Kenya

mzima na ataweza kuangalia masirahi yote ya wananchi wa Kenya. Na ningependelea katika hali ya maisha ya President, asiwe

anapitisha umri wa miaka 70 akiwa katika kiti, ili apatiwe vipindi viwili peke yake, ya miaka mitano mitano na ikimalizika naye,

alitae aende akapumzike kama watu wengine.

Na katika hali ya mwisho ya President, ningependelea awe hawezi kuwa above the law, awe ni kama wananchi wengine,

akifanya makosa akiwa office ajihusuru ili aweze kupelekwa kotini mara moja. Ya pili ningesungumza hapa katiba juu ya

wajumbe wa bunge ambao ningependelea wajumbe wa bunge, wakienda bunge kuwe na sheria ambaye italinda waliomchagua

akiwa hafanyi kazi aweze kuondolewa mara moja hata kama miaka mitano haijamalizika.

Ile ingine ningependa wajumbe wasipatiwe nafasi ya kucheza na katiba ambaye tunaitengeneza wakati huu, ati wakienda bunge

kila wakati wanaibadirisha badirisha, ikiwa inataka kubadirishwa, iletewe wananchi wakubari mabadirisho au wakatae.

Ningependelea vile vile kuwe na board ambaye intashughulika na hali ya wambunge isiwe kama vile ilivyo sasa hati wao

wanajipatia mishahara million moja wakati mwalimju anakosa mshahara wa elfu tano. Ningependelea vile vile wambunge

wakati wanapatiwa magari, wapatiwe magari rahisi rahisi ambaye haitatumia pesa za wananchi mingi sana wakinunuliwa Marange

rover na ma-trooper. Wanunuiwe gari ambazo mwananchi wa Kenya ataweza kuidumu kuinunua. Vilevile

ningependelea katika bunge letu lijalo wabunge wote, wawe wakiwatumikia watu na katika utumishi wao vile vile nao wapatiwe

vipindi ambavyo wanaweza kukaa kwa bunge, nayo hiyo ni kutoka miaka tano hadi kumi na tano. Jambo lingine hapa,

ningesema katika local government ma-councillors nao wanafaa waangaliwe na katiba mpya wapatiwe mshahara ambao

wataweza kudumu na kuelimisha watoto wao maanake wakati huo anapatiwa sijui elfu kumi wakati mbunge naye anapatiwa

elfu kama 500 na marupurupu juu yake. Ma-mayor nao ambao wanaongoza city zetu za Kenya, inafaa wawe wana elimu ya

kutosha na zaidi wawe wana elimu kutoka ya university ili waweze kuendesha city zetu za Kenya na jia ambao ni nzuri.

Ma-councillors nao wawe ni watu ambao wana elimu ya kutoka form 4 ili vile vile nao wawe wakielewa ni wapi mambo

yanaendelea. Katika utumishi, kusiwe na ugawanyishi wa majimbo katika nchi yetu ya Kenya, ili tuweze kuishi pamoja kama

dugu lakini county councils zipatiwe nafasi yakutumia rasrimali zao ili waweze kuwasaidia wananchi wa council yao kwa vile

mapato wanapata kule.

Langu la kumaliza niseme wananchi wa Kenya katika katiba mpya waangaliwe maanake wakati huu wana shida sana na hizi

pombe za kienyeji, wana shida kwa kunya pombe za kienyeji na kushikashikwa kila siku, katiba iwaangalie kama ni pombe hizi

za bei rahisi zitengenezwe kiasi ya ili nao waweze kufurahia kunywa kama vile matajiri wanafurahia kunywa chupa moja Hilton

ikiwa inatoka shillingi mia tatu.

Na mwisho commissioners wangu, nimefurahi na ninashukuru ya kwamba, katiba mpya itaweza kusimamia wanakenya ili

waweze kuishi kwa maisha bora. Asante.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!