ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
79

mambo ya mali, ningetaka serikali, isaidie watu na, tulipa pesa yeyote ya maji, tungetaka hata serikali ijengee watu hii storage

tanks ya maji, ili ikikuwa ni wakati ya kiangazi, wawe wakitumia hayo maji. Lakini ningetaka hata hiyo serikali, itusaidie na

kuchiba hiyo misima, ile ya chini ili watu wapate maji ya kutosha.

Mambo ya Education – tungetaka education iwe free from standard one mpaka standard 8. Tungetaka iwe free na hata

ikakataa kuwa free, iwe garama inagawanywa na iwe kidogo.

President – President naye asiwe over law na awe kwa vipindi viwili tu.

Parties – Ningetaka vyama viwe chache kwa sababu ingine watu wanatafuta tu pesa. Iko zingine hazipati hata mjumbe kwa

parliament au councilor, sasa wengine wanaendelea kukaribisha hiyo vyama ili wapate pesa. Tungetaka naye kiwe kidogo.

Ushirika – vyama vya ushirika, tungetaka mtu yule, kwa sababu vyama vya ushirika wengine wanakula pesa, hakuna pesa

wanapunguza, tunaktaka mtu yule atakula pesa ya ushirika tena ashitakiwe, afungwe, akifungwa, akirudi, ashitakiwe tena na

kama ni mali yake yauzwe.

Asante sana.

Com. Ratanya: Asante sana Kaberia, pengine kuna swali. Hakuna swali kwa hivyo enda usign register. Na kama una

memorandum ungetaka kupeana tungeshukuru. Na anafuata ni Jeremiah Mwiti.

Jeremiah Mwiti: Asante kwa viongozi ambao wako mbele yetu, na jina langu naitwa Jeremiah mwiti. Sheria kifungo ile

inasimamia, Barbara tunataka ichunguzwe sana kwa maana yule mwenye kupewa kadarasi, iko mahari saa ingine anaficha ama

anatua. Iko njia zamani, mzungu akiwa hapa kulikuwa na njia ya watu ya mguu, na njia ya maji, na njia ya gari. Hakuna maji

iliokuwa ikienda kwa shamba la mtu halafu aende afunge. Hio sheria kama ingeolekebishwa, ama ilituwa iangaliwe sana

iwekwe kwa huyu mwenye kuweka kadarasi hiyo ya barabara, hatumii vile sheria ama vile barabara inatakikana.

Ya pili, President hatakiwi kuwa overall kwa maana akiwa overall anaweza kuua hata mtu akakosa kuwa huru.

Com. Ratanya: Overall ni kama kusema je Unaweza ata kusema kwa Kimeru.

Jeremiah Mwiti: Asiwe juu ya sheria, kwa maana anaweza kuua mtu ama kusema watu wanyongwe wote katika Kenya na

hakuna mtu atamuuliza.

Hii ingine, Sheria yote, ifanywe na parliament kwa maana tukisema kama sisi wameru tuko na Njurincheke, yule mkisii naye

atasema ingine, huyu mwingine naye aseme ingine. Sheria itakuwa inaharibika. Wacha sheria yote tupeleke kwa parliament kwa

maana tuko na wajumbe kila nchi hapo. Utadi wote uko parliament kwa maana sasa nikisema Njurincheke ndiye inafaa

kufanya sheria, mkalenjin naye aseme hiyo tutaharibu sheria.

Kwa Kenya yetu, tuko na President, President akiwa mwanamme, mdogo yake awe mwanamke, kwa maana naelewa