05.01.2015 Views

ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet

ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet

ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

42

Com. Abubakar Zein: Asante sana mzee Ratanya, habari ya asubuhi Kama mlivyo ambiwa, mimi naitwa Abubakar Zein, ni

commissioner kutoka tume ya kurekebisha katiba Kenya, na ningependa kuongezea kidogo tu alioyasema Mzee Ratanya ili kazi

yetu iwe ya rahisi, na iwe na nidhamu. Katika kuongezea, ulipoingia hapa pale nje ulikuta kuna mtu anaadikisha majina, sio

Sasa yale majina huandikwa kwa number na sisi tutafuata orodha hiyo kufuata majina na mna hiyo. Ukiitwa jina lako,

unatakikana uje ukae hapa, ushike microphone, utaje jina lako kabla hujaanza kuzungumza, na ni mhimu sana wewe kutaja jina

lako, kwa sababu gani Huyu binti mliojurishwa kwenu anainua mkono, kazi yake yeye ni ku-record mazungumzo yote

anayozungumzwa hapa kwa tape recorder, ndio tusipoteze hata neno moja. Ndio saa ingine ukiona saa ingine hatuandiki,

ukasema hatuandiki, ukasema hawa namna gani maneno nasema lakini haandiki. Kila neno tuna-record na tutaliandika chini

tukishafika Nairobi wanaendelea na kazi hizo Nairobi. Na kama alivyosema Mzee Ratanya, karatisi unaotupa kila kitu

tutasoma, kwa hivyo usiwe na wasi wasi kuhusu maneno mengine yatapotea. Ndio maana tuna-record hayo maneno, utaje jina

lako na uzungumze ndio awe na record vizuri.

Lingine la mhimu kufahamu ni kwamba, juu ya kwamba umepewa uongozo wa lugha, lakini kuna muongozo mwingine wa lugha

kule kwetu Mombasa wanasema, watu wakisumza katika hadhala kama hii, kikao kama hiki, wanatakiwa watumie lugha ya

muluwa, yaani lugha ambayo haitamkasirisha mtu yeyote, kama mzee yuko pale ukitumia lugha hio aone ni lugha ambayo inafaa

kutumika mbele ya wazee. Kama mama yuko hapa, utumie lugha ambao inaweza kutumika mbele ya mama. Kwa hivyo ni

lugha yenye heshima ambayo haitumii matusi.

Kitu kingine, kwamba masungumzo unayozumza hapa, maoni unayotoa hapa wewe unalidwa kisheria, sheria hii iliounda

mabadiriko ya katiba, inakulida wewe kikamirifu, hautachukuliwa hatua yeyote kwa maoni unaozungumza hapa. Kama tulienda

kwingine wakasema, sasa nikisema maneno mengine, yakikasirisha mtu fulani au kasisi fulani, au chama fulani, au office fulani, si

nitapata taabu Tunasema hapana, hakuna atakayekasirika, akikasirika atamezea hivo hivo tu na hasira zake lakini hakuna

hatua unaweza kuchukuliwa wewe. Sijui kama tunaelewana hapo, lakini hiyo haina maana, unajua nchini kwetu tunasungumza

habari ya uhuru, kama sasa huo ndio uhuru wa mwananchi kuzungumza maneno yake kwa uhuru, hio haina maana. Uhuru

hauendi bila kuhajibika, au haina maana hiyo Hatutakubali mtu hapa kuja kuanza kutukana mtu mwingine, aseme mtu fulani, ni

hivi na hivi, hii mambo ya kubadilisha katiba hayahusu watu. Tunataka mapendekezo yako kuhusu katiba. Kama alivyosema

commissioner mwenzangu, unaweza kuwa na malalamiko miingi lakini hayo malalamiko, hayatatusaidia sisi ikiwa hautatwambia

tunapendekeza hivi na hivi na hivi kutatua matatizo haya. Kwa hivyo hatutakubali kuingiliana watu kuchafuliana majina, au

kutukana wengine, na mtu akifanya hivyo tutamsimamisha tuseme subiri.

Lingine la mhimu kufahamu, ni kwamba kama alivyosema Commisisoner Ratanya, tutakaa hapa mpaka jioni, na tutatumia list hii

lakini sisi lakini sisi huwaomba ruhusu wananchi kama nyinyi mbele kwamba kukiwa kuna sababu za kutosha, sisi kutokufuata

list hii, tumuite mtu ambaye pengine hayuko kwenye list, au juna lake liko mwisho kwa sababu za kutosha. Kwa mfano, aje bibi

mmoja hapa mja mzitu, na hawezi kusubiri kwa mda mrefu kukaa chini, sijui kama mtatupa ruhusa bibi kama huyo apewe nafasi

asungumze aende nyumbani.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!