05.01.2015 Views

ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet

ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet

ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

137

Jambo lingine tungependa kuwashukuru wale wote waliofanya kazi hii waweze kuwa ni kazi imefanyika vizuri kwa shukurani

zetu nyingi sana kwa headmaster wa shule hii, kwa kuweza kutukalibisha hapa ingawaje elimu inaendelea, tukaweza tukapewa

darasa kama hili, tukafanyia kazi hapa na pia tunashukuru sana kwa headmaster kuwaruhusu wanafunzi pamoja na waalimu kuja

kutoa maoni na ni muhimu sana kwa watoto kama wale kutoa maoni na tumeshukuru sana Bwana headmaster, kazi hiyo ni

nzuri. Na pia tunamhakikishia ya kwamba tutaandika mwisho, kila mahari tulipata usaidizi na kila mahari tulifanyia kazi yetu

tutaandika katika historia ya Kenya, kwa hivyo shule hii na watu wa hapa wameshaingia kwenye historia kwamba walihusika

katika kubadirisha katiba yao. Halafu pia tungeweza kuwashukuru wale wengine waliochangia kwa njia moja au ingine na

kuhalifu kwamba leo tumefanya nusu ya sehemu ya hapa, ya wakilishi bungeni Tigania East, kesho tutafanya kikao kingine,

jumatato, Muthara Polytechnic Jumatato, Ikiwa sasa ulikosa fursa hapa, au pengine ulikuwa hujajikaza moyo kuwa tayari kutoa,

au una wenzako ambao walikuwa hawajapata habari, waje kule Muthara Polytechnic watakuwa na fursa ya kutoa maoni yao.

Halafu ningependa kuwashukuru wafanyi kazi wetu, nimeona wamefanya kazi kwa bidii, hata mtu alipopotea tunajaribu hivo

hivo tunang’ang’ana, tumekuwa na hao kutokea jumatatu mpaka leo ijumaa, pengine kesho na jumapili ndio watapumzika halafu

tuaanze tena. Na pia ningemshukuru sana commissioner mwenzangu mzee wa huku, huyu ni mzee wa Njurincheke, na

amenikaribisha vizuri, hata nimeaanza kufundishwa kimeru kidogo kidogo. Sijaweza kuanza kula miraa lakini nimeanza

kufundishwa kimeru kidogo kidogo, jinsi ya kutamka maneno, na majina ya watu, na nina furaha kubwa sana nimekaa vizuri

hapa na hata wafanya kazi wetu wana furaha tumekaa vizuri, tulikuwa pande za maua huko, Igembe, tukaenda Ntonyiri, sasa

tumefika hapa. Ningependa kumpa fursa hii, mwaakilishi wetu ili atoe mambo anayotaka kuzungumzia na pengine kama kuna

watu anataka kuwashukuru, halafu akimaliza aite mmoja wetu atuongoze kwa maombi halafu akiturudishia sisi chombo hichi

tutafunga kikao hiki lasimi.

George Kimanthi: Asante sana Commissioner Zein, asante sana commissioner, mimi sina mengi ya kusema ila tu

nitamshukuru nyote kwa kujitolea kwenu kutoka asubuhi tulipokuja hapa, tumeona katika sehemu zote za Mikinduri, na

nimeona vile mmepeana maoni mazuri, kwa hivyo ningetoa shukurani nyingi sana kwa sababu ya kujitokesha kwenu. Saa hii

nitawashukuru macommissioner kwa kujitolea kwao, tumekuwa na hao tangu asubuhi, na sasa jumatatu tumekuwa na hao

mpaka Nyambene, mimi sina mengi sitarudia kwa vile amesema lakini nitasema ya kwamba, kama alivyo mwambia, jumatatu

tuko Muthana Polytechnic, na kama kunaye ana msoana anaweza kwa office yangu, office yangu iko county council, county

council Maua, mwajua pale iko Kwa hivyo kama kuna mambo, kuna watu ambao wamewachwa na wako na maoni labda

wangetaka kuandika, wanaweza andika na watuletee hapo, tunaweza tuma Nairobi ama tupeleke sisi wenyewe. Kwa hivyo

hatujafunga kabisa kuleta maoni ya watu, tunaendelea mpaka, kabla mwezi wa nane, kama vile commissioner amesema.

Jambo lingine ambalo ningetaka kuwakubusha, wale wanasomesha elimu ya uraiya, civic education providers, ni kwamba tuko

nao, hatuja ______ kabisa. Huu sio mwisho wa kulekebisha katiba, sasa mkubuke ya kwamba commission itakusanya maoni

ya wananchi katika eneo la wakirisho ______________ maoni pamoja, halafu itoe report, na hii report lazima italetwa kwa

wananchi tena ili musome hiyo report na muone mapendekezo yenu ya kurekebisha katiba, na kama kuna ye atakuwa na swali

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!