ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
40

Roselyn Nyamato - Programme Officer

George Kariuki - Asst. Programme Officer

Zipporah Wambua - Verbatim Recorder.

George Kimanthi - Co-ordinator

Jimmy Muketha - Chairman

George Kimanthi: Leo tuko na fulaha kubwa hapa Mikinduri, vile tumekuwa tukimwambia, leo tuko na commissioners,

tumekuja hapa Mikinduri kuchukua maoni yenu, nitamueleza majina yao baadaye lakini ningeomba kwanza tuanze na maombi,

mmoja wenu atuongoze kwa maombi.

Mr. Kubai: Natuombe, Baba wetu uliye binguni, tunakushukuru baba kwa kutuwesesha kuona huu mchana wa leo, tena baba

yetu kufikisha hata wageni wetu hapa Mikinduri ili kuongoza hali hii kulekembisha katiba, Mngu baba wetu tunakuomba baba,

wewe ndiye unachagua wafaume ama viongozi, baba tunakuomba utuchagulie kiongozi anayefaa kutuongoza baba.

Tumeteseka na ufisadi, na rushwa baba tunakuomba, kiongozi utakayemchagua akomeshe rushwa akomeshe ufisadi, ili baba

watoto wetu wapate ujira, baba wetu uliye binguni, yeyote atakayeongea leo hii hapa Mikinduri, baba mpe nguvu na uwezo ya

kuongea yale yatawezesha hii katiba ya Kenya kuweko kwa njia nzuri, baba wetu tunaomba kwa Kenya nzima, baba kuna

magojwa mengi, shida nyingi za ukosefu wa kazi, na kadhalika. Baba tunaziweka mikononi mwako, ili yeyote atakayeongea

aongee akiwa umemjaza roho wako mtakatifu. Twakuomba hayo machache tukijua baba utatukamilishia kwa jina la mwana

wako bwana wetu Yesu Kristo. Amen.

George Kimanthi: Asante sana bwana Kubai, kwanza kabisa mimi naitwa George Kimanthi. Labda kuna wengine ambao

sijawai kutana na hao hapa lakini nakubuka nimekuwa katika vikao mingi hapa, kuona kazi yenu huko _____ (inaudible). Ni

kawaida yetu kutabulisha wale tuko nao katika kila mikutano. Naona hapa tuko na chairman wa committee Mr. Jimmy

Muketha. Halafu tuko na mwingine, wengine hawajafika, kuna wengine kwao ni mbali sana kama huko _______(inaudible) na

kuna huyu mwingine ako hapa nje, Isaiah King’eru, mnamjua Kwa upande huyu tuko na commissioners kama vile

tumemwambia, tuko na commissioner Zein Abubakar, halafu tuko na commissioner Domiziano Ratanya. Hapa tuko na

prorgramme officers, tuko na Roselyn Naymata, halafu tuna Mr. George Kariuki, na Zipporah Ndunge. Hawa ndio tuko nao

leo kuchukua maoni yenu kwa sababu hii ndio ile stage mhimu sana katika hii shughuli yetu ya kulekebisha katiba ya Kenya.

Kwa hivyo mimi leo sitakua na mengi ya kusema, nataka tu kumuomba mshikilie yale watakaomwambia, watamueleza vile

wanataka nyiny mtoe maoni yenu. Langu ni kumuomba tu muwe watulifu, msipige makirere, mfuate ile mtakaoambiwa, ile

talatibu mtakaopatiwa mfuate sababu kama mnajua watu watakua wengi sana hapa na ukiambiwa uchukue dakika tatu ama ni

mbili, ushikilie hapo usije kukaa hapa sana, kuongea saana kwa sababu kila mtu anataka kupewa nafasi ya kuongea. Si ni hivo

Kwa hivyo nitamuomba Commissioner Damiziano Ratanya ampe ule utalatibu mtakaofuata na atamueleza zaidi kile wangetaka

mfanye kama wananchi wa hapa Mikinduri.