ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
ON 17TH MAY, 2002 - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
72

Mirungi Atunus: Asante sana kwa mwenyekiti. Kwa majina naitwa Atunus Mirungi kutoka upande wa Ngania. Jambo langu

nataka lisiwe maanane ni hii na zungumzia. Mara mingi tumesikia ya kwamba ati serikali inapeana masomo ya bure kwa

wananchi na hivyo sio ilivyo. Kama upande wa primary school, tumesikia ati serikali ilipeana masomo ya bure na tukiendelea na

haya maneno, tunaangalia pande ya waalimu wa nursery school wanalipwa na wazazi na hiyo inakuwa na shida mingi sana kwa

upande wa wazazi. Kwa maoni yangu nataka kama mwalimu wa nursery school awe ameajiriwa na serikali na isiwe maanani

kwa sababu, na akiajiriwa lazima awe na experience na qualification ya college kama waalimu wengine na awe ameajiriwa na

serikali sio wazazi.

Jambo langu la pili, nazungumzia kuhusu hawa vijana wanaambiwa wanatia wasichana wa wenyewe mimba na wakawaacha.

Ile jambo yani ninataka kusema hivi, kama vijana anaenda kwa mzee fulani, atie msichana miimba, na aende, serikali imchukulie

hatua, kama ni huyu kijana akikataa kuoga huyo bibi alee huyo mtoto mpaka wakati umri wake ufike wa kuchukua kitabulisho.

Maoni yangu mengine mwenyekiti, nasema ya kwamba, twende upade wa uchaguzi, kama ni ile contact zinapeanwa kwa

ukalabati, tumesikia ya kwamba pande fulani kuna ukalabati inafanywa na mtu fulani. Hayo nami nataka kuyatia maanani ya

kwamba, mtu akipewa kazi ya ukalabati, awe na qualification ya kutengeneza hiyo ukalabati, sio experience ya pesa. Naona

kuna wale wako na qualifications lakini hawana pesa za kwendesha hiyo nini

Jambo la tatu, nataka pande ya President, p

Com. Ratanya: Goja kidogo, kuna watu ambao wanapiga kelele huko nje, mnajua mkiendelea namna hio itaingia kwa record

yetu hapa. Kwa hivyo mnyamaze. Kwa hivyo endelea Atunas.

Murungi Atunus: Kwa upande ya President, nataka serving President awe ako na sada ya degree na sio sada ya kupandikwa.

Na upande ya bunge, mtu achaguliwe akiwa na umri wa miaka arubaine kwenda 75 na upande wa udiwani, local authorities,

awe na elimu ya O’ level na nataka ata wale ambao wamechaguliwa wakiwa chini ya form 4 wasiruhusiwe hata kuomba kula

kwa uchaguzi ujao

Jambo lingine langu na la mwisho, naongea kuhusu hii mambo ya administration, upande wa chief, chief awe amechaguliwa na

watu kwa mlolongo na awe amefikisha kiango cha O’ level na pande ya serikali, askali akishika mtu, sio lazima aweke kwa

kambi kwa sababu ako na mabrother, ashike mtu apeleke yeye kwa koti mara moja sio kuweka mtu kwa cell. Kwa hayo

machache namalizia hapo.

Com. Ratanya: Asante sana Atunas kwa hayo machache. Sasa kuna Kobia Ritari Isaiah.