TUESDAY, JULY 9TH, 2002 - ConstitutionNet
TUESDAY, JULY 9TH, 2002 - ConstitutionNet
TUESDAY, JULY 9TH, 2002 - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
asiongeze mwingine. (laughter)

Com. Asiyo: Asante sana. Hebu jiandikishe pale (inaudible) pole pole sio shida wewe weka tu. Ukisema msichana asizae

mtoto mwingine, kama wanaume wangekuwa wanazaa dunia ingejaa leo. Kwa hivyo usikate shauri kwa wasichana waki

…unaweza weka meathali umalize hapo. Asante sana sasa tunataka kumsikiliza mzee Harun Kandie. Tafadhali fika mbele kwa

mambo machache sana kwa maana naona una karatasi hapo. Kwanza sema majina yako yote ili ishikwe na machine halafu

uongee kwa muda mfupi sana kama dakika tatu.

Harun Kandie: Asante sana Commissioner, na Commissioner mwenzako. Kwa jina ni Harun Kandie. Yangu ninaenda

upande wa uongozi kwa upande wa machief ile style tungefuata. Style ile tungefuata kwa upande wa machiefs kuandika zamani

wamababu zetu, walikuwa wanaendea kwa elders, kujua ni nyumba gani inastahili kuongoza wananchi. Na ilikuwa mzuri. Hiyo

njia ilikuwa mzuri kwa wakati huo.

Com. Asiyo: Sasa kwa wakati huu unataka wapigiwe kura au wafanye namna gani?

Harun Kandie: Ile kitu ilikuja kuharibu Bwana Commissioner ni kuwa wanasiasa walikuja wakaingilia hiyo kitu, so

wakaharibu ikawa baya.

Com. Asiyo: So unapendekeza namna gani?

Harun Kandie: Napendekeza iwe wazee elders, wawe watapewa jukumu ya kuangalia kama ni chiefs ama ni assistant chiefs

wanagaa chini katika vijijini na kuona ni mtoto wa nyumba gani inafaa kuongoza sisi.

Com. Asiyo: Hao wazee hawawezi kupewa kitu kidogo halafu wachague mtu (inaudible)

Harun Kandie: Zamani ilikuwa hakuna hiyo walikuwa wanaongoza tu.

Com. Asiyo: Zamani hakukuwa na kitu kidogo. Na sasa?

Harun Kandie: Hii kitu kidogo ndiyo inaharibu mambo.

Com.Asiyo: Sasa tutafanya namna gani?

Harun Kandie: Wazee walikuwa wanajua ni nini wanaendelea na wazee wakigaa wanao mambo yao ya ndani.

Com. Ayonga: Sasa hao wawezi kuonea nyumba fulani tu ndiyo inafaa kuwa inatawala na hali nyumba ile haitagawana?

16