TUESDAY, JULY 9TH, 2002 - ConstitutionNet
TUESDAY, JULY 9TH, 2002 - ConstitutionNet
TUESDAY, JULY 9TH, 2002 - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Com. Asiyo: Mpaka miaka kumi na nane? Sasa sema ya mwisho.

Harun Kandie: Ya mwisho ningeenda upande wa siasa. Hii watu wetu wa siasa. Siku hizi wanaenda parliament wiki mzima.

Zamani wakati wa ukoloni sisi tulikuwa vijana Mbunge alikuwa anakuja, ikifungwa parliament anakuja mahali kwa wananchi

kuchukua maoni ya wananchi. Lakini siku hizi hatuoni.

Com. Ayonga: Sasa hiyo unataka aje?

Harun Kandie: Tunataka hiyo iwekwe sheria kwa sababu sisi tunaandika yeye.

Com. Ayonga: Weka sheria.

Com. Asiyo: Sasa hiyo sheria ndiyo tunataka utambie sasa mara hiyo sheria yako ndiyo tunataka.

Harun Kandie: Sheria hii yake tunataka wakati bunge hakuna, akuwe na watu wake.

Com. Asiyo: Na kama hakukuja?

Harun Kandie: Basi wananchi watajua (interjection)

Com. Asiyo: Kama hakukuja tupatie sheria hiyo natuandike namna gani?

Harun Kandie: Sasa kama huyu mtu hajakuja inaonekana hajui kazi yake wananchi wata-vote yeye out.

Com. Asiyo: Kwa hivyo (inaudible) ni watu wangapi wanaoweza wanataka huyu mtu arudi nyumbani wachague mbunge

mwingine. Watu wangapi kwa (inaudible)

Harun Kandie: Nikirudi nyuma kidogo kuna mzee ameandika mambo ya (inadible)

Com. Asiyo: Kama mtu hajafanya kazi yake kama Mbunge, na watu hawatosheki unataka Mjumbe mpya unataka watu

wangapi wazee waseme kwa kweli huyu hajafanya kazi yake ndiyo tuwe na mpango ya kufanya recall yaani kurudisha yeye

nyumbani halafu mtu mwingine achaguliwe? Maana kuna fitina mingi kama yule mtu aliangushwa anaweza tafuta watu kumi na

mbili watu elfu moja waandike barua huyu mtu arudi hapa hatujaona yeye hafanyi kazi tunataka aondolewe. Na hiyo imeleta

fitina nyingi sana katika nchi hii ta Kenya. Na wewe unajua fitina ya (inaudible) sasa tuambie unataka tufanye namna gani?

20