TUESDAY, JULY 9TH, 2002 - ConstitutionNet
TUESDAY, JULY 9TH, 2002 - ConstitutionNet
TUESDAY, JULY 9TH, 2002 - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Com.Asiyo: Kwanza jiandikishe pale halafu ukae. Nataka kuuliza kuna mtu moja hapa ambaye angependa kusema kitu

ambaye anaona mtu hajasema? Anaitwa nani? Kitu ambacho hakijasemwa anaitwa Boniface Kimwei. Boniface ulikuwa wapi

wakati huu wote? Hapana hapana tuliita mara nyingi sana.

Com. Ayonga: Sema hicho kitu

Com. Siyo: Kidogo sana na ile haijasemwa

Com. Ayonga: May be majina kwanza.

Boniface Kimwei: Majina yangu ni Boniface Kimwei, ni mwalimu katika hii division. Now yangu ambayo ningpenda

kupendekeza ni kwamba huu, - wakati mtu ako na mali yake kwa shamba lake serikali inaingilia. Hatungependa serikali

iingilie. Mfano wakati uko na mali yako unakuta ya kwamba badala ya wewe ukate ile miti ndiyo wewe utumie, serikali lazima

upate idhini kutoka kwa serikali (interjection)

Com. Asiyo: Hiyoni haki ya serikali na ni vizuri na hiyo ni sheria mzuri sana na tutahimiza hiyo.

Boniface Kimwei: Lakini tungependa kubandilisha hiyo sheria mtu awe ana control mali yake yeye mwenyewe. Jambo la pili ni

kwamba kuna watu ambaye ni disabled, ni viwete. Utakuta wale watu serikali yetu tukufu haizingatii sana. Ningeonelea kwa

maoni yangu ya kwamba serikali yenyewe itenge kiasi fulani cha pesa na ipatiwe katika wizara fulani, ndiyo iwe ikisaidia wale

disabled wawe kama wale Wakenya wengine tuweze kuinua uchumi yetu katika Kenya.

Ya tatu ni kwamba hii sheria inatungwa katika Kenya hii, inaongewa kwa lugha ingine ambayo mwananchi wa kawaida hawezi

elewe. Ningeomba, baada ya kumaliza kutunga sheria hiyo sheria itafusiriwe katika lugha mbali mbali za makabila zetu za

Kenya.

Com. Asiyo: Hiyo tayari imeandikwa na pia itakuwa hivyo.

Boniface Kimwei: Na pia iwekwe mahali ambapo wananchi wanaweza fikia kama District Coordinator awe na moja na

Library (interjection)

Com.Asiyo: Hata huyo alisema itakuwa ofisi yake.

Boniface Kimwei: Jambo la nne ni kuhusu elimu katika nchi yetu. Utakuta ya kwamba elimu katika nchi yetu kila mtu anakuja

na syllabus mwaka huu tunabadilisha hii, mwaka huu tunabadilisha hii, tungependa elimu tuwe na syllabus ingegaa hata miaka

ishirini au ishirini na tano. Lakini si kubadilisha tukifika mwaka huu tunabadirisha ukifika mwana huu tunabadilisha, ukifika

mwaka ule tunabadilisha. Yangu ni hayo asanteni sana.

Com. Ayonga: Kuna neno ambalo tumeambiwa tukoka kila pahali, kwamba usiseme kiwete, si wewe ni mwalimu?

Boniface Kimwei: Yes, Sir.

77