constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
104

Yampat mapelu: Ore naba nasuj ina.

Translator: Yake ile ambayo itafuata hiyo,

Yampat mapelu: Na ene wueji e nkisuma.

Translator: Ni mambo ya elimu.

Yampat mapelu: Ore ene wueji ena sukul ne primary.

Translator: Mambo ya shule za Primary,

Yampat mapelu: Nayieu nai neaku ene pesho.neaku aitabaiki ine pemaigil ta.

Translator: Angependelea iwe ya bure.

Lengete Kamete: Kwa jina naitwa Lengete Kamete. Na sina mengi ni machache mno. Langu la kwanza ningependelea

mambo ya Electoral Commission ama Chairman wa Electoral Commission awe akichaguliwa na Parliament, isiwe tena ni Rais

anateua mtu binafsi. Pia ningependelea mamboya President ama Rais, awe anaweza kuchaguliwa kwa muda wa mihula miwili.

Kwa mfano awe kama miaka kumi kwa ile system iko Kenya sasa hivi. Hiyo system ya mihula miwili, pia Rais awe

akichaguliwa tuseme kwa kabila hii, muhula huu. Muhula mwingine iwe ni kabila ingine. Kwa sababu naona kuna kabila zingine,

Yesu atarudi kabla wengine hawajapata nafasi ya ku-enjoy huo muda. Kwa hivyo pia iangaliwe kwa makabila pia wahusike

ama wawe wakichagua Rais wao.

Com. Lethome: Unasema President achaguliwe kwa kila kabila?

Lengete Kamete: Yes.

Com. Lethome: Na tutafanyaje ili tujue the next kabila ama ni kura inapigwa au tunaenda alphabetical order ili tujue ile kabila

inafuata?

Lengete Kamete: Kwa mfano sasa hivi, Wakikuyu wameshakalia, Wakalenjin wameshakalia, sasa wengine tuseme kama ni

Wakisii ama Wa-Baluhya ama ni Wa-Jaluo ama ni Wa-Maasai, wale ambao wana interest ya kuwa Rais, wasimame kwa kila

kabila. Lakini Wa-Kikuyu na Wa-Kalenjin wasisimamishe mtu wao, zile kabila zingine kama kuna mtu anataka asimame na

wananchi waamue ni mtu wa kutoka kabila gani mzuri.

Com. Lethome: Kwa hivyo watakuja kupewa chance ingine baada ya miaka mia nne. Kwa sababu tuko na makabila arobaini

na mbili mpaka saa hivi.