27.11.2014 Views

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

26

Ya pili, siku hizi Serikali imenyima sisi haki. Kwa sababu wakati tuliandikwa sisi kazini, ichague mtu amesoma kwa sababu kazi

ya bunduki sio lazima usome. Kazi ya kuandikwa kama askari sio lazima usome. Lakini siku hizi Wamaasai wametupwa kando,

hawaandikwi kwa kazi, wanakuja kuandika watu wengine wanasema ni watu wa Kajiado, wanaacha wa Loitoktok.

Tunapendekeza uajiri kama wa zamani, inasaidia. Kwa sababu ukifika area ya Umasaaini unakuta mtu amemaliza Standard

eight, Form four yuko nyumbani. Serikali itusaidie sisi, tujisaidie sisi, tuandikwe kama zamani vile tulivyoandika na tulimaliza kazi

yetu. Hatujasoma lakini hiyo kazi inaendelea vizuri mpaka wa leo tuko kazini. Sasa mimi sina mengi sana kwa sababu niligusia

pahali ya majimbo na pahali ya masomo ndio nafaa nigusie kidogo. Kwa sababu area yetu imeenda kwa sababu tunapatiana

kwa yule mtu ako na hope kidogo. Yule ambaye anaambiwa, ‘nifanye kitu fulani halafu nikupatie kazi.’ Serikali iangalie hapo.

Sasa mimi sina mengi sana, ilikuwa ni hivyo tu na naomba Serikali iangalie kwa mambo hayo.

Com. Bishop Njoroge: Haman Ole Nsuki. Isaiah Ole Samana. Isaiah?

Isaiah Ole Samana: Yangu nitaanza moja kwa moja kulingana na vile nilivyoanza. Kwa majina naitwa Isaiah Ole Samana,

mimi ni mkaaji wa Loitoktok sub-district. Yangu ya kwanza ni kuhusu Provincial Administration ama utawala wa mikoa.

Utawala wa mikoa kwa mapendekezo yangu, ningependa iendelee kudumu. Sababu ni kwamba utawala wa mikoa, hiyo

inaunganisha ama inapatanisha mtu kwa mtu. Utawala wa mkoa unaimarisha maendeleo na kuunganisha wananchi. Ni chombo

cha kuunganisha wananchi na Serikali.

Kuhusu madiwani: Madiwani mimi katika mapendekezo yangu, madiwani wanyimwe mamlaka. Kwa sababu gani? Diwani

anapochaguliwa kuwa diwani, anakuwa na chance ya kunyakua ardhi ama kunyakua plots. Na kwa mapendekezo

ningependekeza kuwe na kamati katika ward ya huyo diwani ambayo itakuwa ikihusika na mambo ya kupeana plot kwa

wananchi.

Kuhusu wafanyikazi: Wafanyikazi wa kila idara, tungependa wawe asilimia sabini. Wawe ni wenyeji wa hiyo sehemu. Kwa

sababu tunaona ya kwamba wafanyikazi wengi unakuta wanatoka katika nje, sio wakaaji wa hii sehemu na wakaaji wa hii

sehemu wengi wao wamesoma. Lakini kwa sababu ya godfathers huko mbele, unakuta wale wenyeji weanakosa kazi. Kwa

hivyo kwa mapendekezo ninaona ya kwamba wafanyikazi wa kila idara wawe wenyeji wa hiyo sehemu. Asilimia sabini.

Kuhusu Land Control Boards: Mashamba: Ningependekeza ya kwamba watu wanapouziana mashamba, waanze katika ngazi

ya chini mashinani. Kwa sababu tunaona ya kwamba watu wengi siku hizi wanauziana mashamba na wanapelekana katika kazi

ya mbele, ya juu zaidi. Bila kupitia ngazi za chini. Watoto hawajui, jirani hawajui, relative ya huyo mwenye kuuza hawajui. Kwa

hivyo tungependekeza hiyo sheria ibadilishwe iwe mawelewano ya kuuziana mashamba ianze huko chini ndio wenyewe wapate

kujua ya kwamba watoto watabakishiwa na sehemu ama huyo mtu asiuze kwa sababu kutakuwa na vile tutaweza msaidia hiyo

ardhi ibaki.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!