constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
9

Constitution. Ambayo katika district, itakuwa tu wakati kura inafanywa elections. Tuwe na Local Authority, kutoka Local

Authority tuwe na Regional Authority.

Com. Lethome: Hiyo Regional Authority itakuwa katika ngazi gani?

Rev. Elias Ntoipo: Unamaanisha nini unaposema ngazi gani?

Com. Lethome: Will it be at the Provincial level?

Rev. Elias Ntoipo: Yes. It will be at the Provincial level.

Com. Lethome: Majimbo will be a Province?

Rev. Elias Ntoipo: It will be a Province. Ndio. Kama Rift nasema kwamba, igawe mara tatu, iwe North, iwe South, na

Central. Hiyo ndio namaanisha. Kwamba ni region, sio katika kikabila. Aah ah - katika wale watu ambao wanakaa katika

sehemu fulani ya given area.

Com. Bishop Njoroge: Asante kwa maoni hayo. Palashina Ole Sunkuri.

Palashina Ole Sunkuri: Mimi kwa majina ni Palashina Ole Sunkuri. Maoni yangu ni kwamba wakati mzungumzaji

alipozungumzia mambo ya nchi kukuja kugawanywa kama sehemu ya Loitoktok hii. Ilikuwa iko kiwango ambayo wale

wataalamu wa zamani walikuwa wanatuweka. Anasema kila mtu ni elfu moja. Lakini wakati huu, sijui vile ilifanyika mpaka

wengine wanapata elfu tatu kwa kazi na wengine wako na zaidi ya elfu tatu. Nikaona hapo ni kama wagawaji ardhi

wananyanyasa wengine. Tunataka kila kitu kiwe sawa.

Kwa sababu kuna watu ambao hawana uwezo na wanaweza kunyanyaswa na wale ambao wako na uwezo. Sasa, kuja hapo

tena kuweka ile tunaita Land Control Board, imemaliza watu kabisa. Ziko familia ambazo saa hii, hakuna hope hata ya acre

moja. Kwa sababu ile kitu inatendeka hapo, tunakuta familia ni Mzee anaenda kuuza shamba, watoto hawajui, mama hajui, ni

karatasi tu tunapelekea Mzee, aambiwe katika hiyo land ambayo alikuwa anaishi. Hiyo tumeona hapo, ni wanyanyasaji

wakubwa kwa sababu hawa wananchi wenyewe wapewe ardhi yao. Waangaliliwe ardhi yao vile wanakaa. Kwa sababu

mambo mengine unaona kama Commissioner wa Land huko Kajiado, hata huyu anaishi Kajiado, hana pesa ya kwenda huko

kulalamika. Wanakimbia hapa hapa tu, kuzunguka kama chura akiwa ndani ya maji na hakuna kitu mtu anaweza kufanya. Sasa

ardhi inaenda namna hiyo. Sehemu moja.

Ya pili, tuko na mila, ambayo saa ingine tunakuwa kama Uongozi.