27.11.2014 Views

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

61

hapa mbele. Hawa ni wanafunzi wa shule na tutawakubali kupeana maoni ili waweze kurudi kwa shule. James Ngugi aje basi.

James Ngugi: Asante sana. My name is James Ngugi, Mwalimu wa shule ya upili ya Ilasit Secondary School na nina maoni

machache kuhusiana na kubadilishwa kwa Katiba ya Kenya. Kwanza nitazungumzia sana hasa kuhusu idara ya elimu kwa

sababu mimi ni Mwalimu. Ningependekeza katika shule za msingi, kuwepo na shule maalum ambazo zitashughulikia wanafunzi

ambao ingawaji sio wazuri sana katika yale masomo ya darasani na ni wazuri katika ile elimu nyingine kama ya ufundi, tailoring

na kadhalika. Kuwe na shule maalum ambayo itaanzia kushughulikia masilahi ya hawa watoto wao kutoka katika shule za

msingi hadi katika vyuo vikuu. Hata kuwe na mitihani ya kitaifa ambayo inahusiana na hiyo.

Hiyo ni ya kwanza. Pili ningezungumzia kuhusu lugha ya Kiswahili na ningependekeza ya kwamba lugha ya Kiswahili iwe

inafundishwa ama iwe ni somo la ufundishwaji kutoka katika shule ya msingi hadi vyuo vikuu. Hata vyuo viweke ile ndio ili

kuleta ushikamano na ili kuleta hali fulani ya umoja katika nchi hii ya Kenya. Kwa hivyo kufungamana na hayo, ningependekeza

ya kwamba kuwe na chama fulani ama kuwe na idara fulani katika wizara ambayo itahusiana na kuleta mbinu fulani ama

mitakati fulani ambayo itachangia katika kuhakikisha ya kwamba Kiswahili kinafahamika na kila Mkenya.

Ya tatu ningependekeza ya kwamba hizi shule za kitaifa, zilikuwa chache sana na hizi shule kwa maoni yangu zilichangia sana

katika kuleta ya ushikamano Kenya nzima na nikechangia ya kwamba hizi shule ziongezwe. Kwa sasa tuna shule kumi na nane

tu za kitaifa hapa Kenya na tukiangalia hata katika wilaya hii, hakuna shule hata moja kama hiyo ya kitaifa. Na ningependekeza

shule hizi ziongezwe kwa kupitia Wizara ya elimu, ihakikishe ya kwamba zitakuwa nyingi zaidi. Angalao kila wilaya kuwe na

shule moja ya kitaifa. Halafu nikizungumzia kidogo kuhusu vyuo vikuu, ningependekeza ya kwamba wale Vice-Chancellors ama

wale wakuu wa vyuo hivyo, ningeomba ya kwamba, isiwe Rais wa nchi ndiye ambaye ndio kiongozi pale. Bali iwe ni kiongozi

msomi wa pale chuo kikuu. Kwa sababu inakuwa ni vigumu sana kuingilia au kuchanganya siasa na uongozi. Kwa hivyo

ningependekeza ya kwamba hawa wawe ni wasomi ambao wanachaguliwa na wale wasomi katika chuo kile.

Halafu pia ningependa pia kuzungumzia kuhusu swala la waalimu na ningependekeza ya kwamba mishahara ya waalimu pamoja

na marupurupu yao na hali zozote zile za kikazi, zishughulikiwe na Katiba ambayo itakuja sasa. Iwe ya kwamba, maongezi ama

mapatano yeyote kati ya Serikali na vile vyama vya waalimu, iwe ni kama sheria na isiwe inaweza kubadilishwa kwa hali yeyote

ile.

Halafu nikimalizia ningependa kuzungumzia pia kuhusu somo la Katiba. Ningependekeza kwamba pawe na somo la Katiba

kutoka katika shule ya msingi. Ndio ili watu waweze kujua nchi yao. Kuna mifano mingi sana ya watu ambao hawajui nchi yao,

hawajui namna nchi inavyoongozwa. Hawajui mambo ya haki yao na ningependekeza ya kwamba kuwe na somo la Katiba ama

somo la Serikali - jina lenyewe, wale ambao wanahusika wanaweza kutoa jina nzuri. Iwe inaanzia katika shule ya msingi hadi

kufikia katika vyuo vikuu. Asante sana.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!