27.11.2014 Views

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

44

Ma-Chiefs: Nafikiri Ma-Chiefs, ninaweza kusema ya kwamba Ma-Chiefs wakae vile walikuwa wakikaa na wawe ni wale

Ma-Chiefs ambao wamechaguliwa katika ile sehemu ambayo wananchi wamezaliwa hapo. Awe ni wa hapo. Sio kwamba

tunaweza kupendekeza iwe eti ni watu wa kwenda transfer. Hiyo hapana na sasa wawe ni wale ambao ni wananchi katika ile

sehemu. Kwa hivyo kwa hiyo ninasema asante sana, sina mengi sana ila tu, niongeze ya kwamba, Serikali ibadilishe hayo

mambo kwa njia ambayo inafaa. Kwa hivyo asante sana, mimi sikuwa na mengi.

Com. Lethome: Asante sana. Jiandikishe. Daniel Molunkei.

Daniel Molunkei: Kwa majina naitwa Daniel Molunkei, mkaaji wa Loitoktok. Kwanza ningependa tu kuzungumzia mambo

ya Administration. Kwamba Administration ibaki vile vile na kuwa na PC, DC, hadi ngazi za chini za Chiefs, na Assistant

Chiefs. Ila tu, ni kwamba iangaliwe Review Act ya uajiri wa Ma-Chiefs kwa kuwa tunaona ya kwamba wakati wakitangaza

kuajiriwa kwa Ma-Chiefs. Unakuta ya kwamba hawafuati ile sheria, wengine wengi hapa katika eneo hili letu ni kwamba

tumechaguliwa Ma-Chiefs ambao hata hawajui kuandikia mkubwa wake Bwana D.O. ripoti, ambao ni aibu kubwa sana. Sijui

hiyo sheria mchunguze muangalie ni wapi kumekosewa. Kwa upande wa Ma-Chiefs pia, tungelipenda sheria ile ya zamani ya

miaka zilizopita ya kwamba Ma-Chiefs wawe wakichaguliwa na raia wao katika eneo lao.

Lingine ni mambo ya masomo, limezungumziwa zaidi lakini kwa upande wangu na maoni yangu, ningeonelea tu kwa mambo ya

marks. Ya kwamba irudishwe ile sheria ya zamani ya kujaribu kuangalia zile remote areas na marks za watoto wa remote areas

an wale amao wanaishi katika rural areas zipandishwe. Isiwe mtoto anafanya K.C.P.E na marks zake zitakuwa ni sawa na yule

ambaye ako Nairobi. Kwa upande pia ya waalimu, itafutwe sheria ambayo ilikuwa hapo awali. Sijui imepotelea wapi, ya public

funds mis-use ambapo Ma-Headmaster wengi wametumia fedha za shule na shule kuadimika. Na nafikiri hiyo ndio imeleta

shida nyingi ya hapa watu wengi wanaanza kusema mashule na vitu kama hizo. Turudishe zile sheria za zamani.

Mambo ya health: Health pia tungeliomba iwe completely free kama zamani ila tu in-patients waweze kulipa yale madai kidogo

tu ya kitanda. Lakini kila kitu mpaka madawa iwe ni huru. Pia sheria iangaliwe ya kuanzisha mambo ya clinics, hizi private

clinics. Imekuwa kwamba watu wegni wameanzisha tu private clinics. Unakuta ya kwamba kuna mtu ambaye yeye ni daktari

mkuu na ameruhusiwa katika ki-profession na sheria lakini anatumia watu wengine ambao sio professionals wa kuweza

kuendeleza ma-private clinics. Kwa hivyo tungeliomba sheria hiyo ya Ministry of Health, iangaliwe kwa maakini kwa sababu

tuna mahospitali ambazo ni duni na kulingana na mambo ya utajiri ama mambo ya kipekee tuna shida hizo.

Ya pili ni mabmbo ya K.W.S., ningeliomba sheria za zamani ziweze kuwa kwa sababu K.W.S. ni parastatal na sheria za

wanyama wa pori ambayo iko katika Ministry of Tourism, iangaliwe irudi hasa kwa upande wa compensation. Compensation

tulikuwa tunalipwa fedha na nafikiri kulikuwa na sheria ambayo ilikuwa imewekwa. Hapa mtu akiuawa na wanyama kama vile

wale wa mbele walisema hakuna fedha ambazo wanalipwa. Mashamba hailipwi.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!