constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
53

ndio wanajua shida za wananchi wao.

Soko huru imeumiza umma. Kwa hivyo hiyo soko huru ifutiliwe mbali. Ma-Chiefs wawe lakini wachaguliwe na watu wa eneo

lake. Sio Bunge. Kwa sababu kunaweza kuwa kuna mpinzani, atachagua mwenzake na pengine hajaridhisha umma. Kwa hivyo

Ma-Chief wawe lakini wachaguliwe na umma.

Hospitali: Tuna shida ya mahospitali kwa sababu madaktari wetu wakuu wanafanya biashara. Unakuta daktari mkuu wa

hospitali, anakuandikia madawa ya kwenda kuchukua kwa clinic fulani. Kumbe ni clinic yake. Kwa hivyo iangaliwe mfanyi

biashara na muhudumu wa umma.

Com. Bishop Njoroge: Unataka kusema ya kwamba, madaktari wanaofanya kazi kwa mahospitali ya Serikali wasikubaliwe

kuwa na clinics zao?

Ibrahim K. Kailepi: Wasikubaliwe kuwa na clinics zao. Wanaumiza umma na waalimu wasikubaliwe wawe na biashara zao.

Asanteni.

Com. Bishop Njoroge: Thank you very much. Joseph Kulare.

Joseph Kulare: Kwa majina ni Joseph Kulare kutoka Ilasit Loitoktok. Nikizungumzia hoja ya kwanza ni kwa President.

President apunguzwe madaraka yake. Asiwe na madaraka ya juu zaidi kwamba akitaka kuvunja Bunge, anavunja tu bila taarifa

yeyote. Ma-Chiefs, MPs, wawe wakichaguliwa na wananchi na wahudumu kwa muda wa miaka mitano ndio wafanyiwe

elections. Hata President asikae kwa muda wa miaka kumi. Iwe full term. Mambo ya culture: Culture itupiliwe mbali kabisa

especially Wa-Maasai wenzetu wanasoma kutoka form one, form four, wanaenda mambo ya ukarani, na hawa Ma-MPs

wanatumia hawa makarani ku-succeed, kupitia kura daraja ya kwenda Bungeni. Pia the formation of the Government:

Tunataka Serikali ya Majimbo ili Serikali iwe na uwezo wa kuangalia watu katika eneo hiyo na wajue idadi ya watu walioko

katika eneo hilo. Especially ya kwetu Loitoktok, sijapendelea sehemu zingine ziwe hivyo lakini kama kwetu Loitoktok, tuna

watu kutoka Tanzania, Rwanda, Burundi, wamepotelea huko for ages na huyo mtu akifa analeta shida. Hujui huyo mtu ametoka

wapi na haujui alikuwa mharifu kutoka nchi fulani ndio akahamia upande huu. Kwa hivyo tuwe na formation ya Majimbo. Ikinge

wale wenyeji wa hizo sehemu za hapo karibu.

Land Act: Mashamba mimi nafikiria kwa council isiuzwe bila kupitia kwa familia iwapo tu kuna shida ya dharura ambayo

ingefanywa waweze kuuza hiyo shamba. Kwa ajili mashamba unakuta inauzwa maofisini, iki-signiwa tu na yule karani wa land,

unakuta familia haijui mtoto wao ameuza shamba. Ukienda kwa Chifu, Chifu anakwambia wewe angalia ile sehemu yako

uliachiwa, wacha huyu ale mali yake. Kwa hivyo Chiefs nao wasiwe na powers, kuwa na Kangaroo courts katika ofisi zao.