constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
59

Serikali ifikirie wale hawana kwa sababu kuna watu wanarundikana kwa railway line, hii reserve. Hiyo railway line ambayo ni

reserve iko na railway, watu wanarundikana huko hawana mashamba na sio kupenda kwao. Zilinyakuliwa na wale wenye

mamlaka zamani.

Lingine mtu kama awe tortured na ichunguzwe ionekane hakuwa na hatua, huyo mtu anakuwa compensated kwa sababu labda

ni madai ya uwongo na rushwa ilitendeka labda pale. Kwa hivyo yangu ni hayo tu.

Com. Bishop Njoroge: Hebu nikuulize, si ni heri ku-recommend kwamba kusiwe na torture. Mtu akishikwa anapelekwa

mahakamani kuliko baadaye. Kwa sababu hiyo ni rahisi. Mtu akishikwa anapelekwa wapi? Mahakamani. Si hivyo ndivyo

ilikuwa? Sawa. Nenda pale. Let’s have Benjamin S. Masharen, headteacher. Karibu.

Benjamin S. Masharen: Asante sana Mwenyekiti, ningependa pia kutoa maoni isipokuwa mambo haya ya Katiba ni magumu

sana na yanakuwa na detail yaani mambo yanaenda ndani sana lakini hata hivyo nitajaribu kutumia wakati mchache sana kwa

sababu mimi ni Mwalimu wa historia. Nikisema ni ku-lecture itachukua muda mrefu sana.

Jambo la kwanza muhimu zaidi ni kwamba mimi niko proponent au kwa kinaganaga, mimi naunga mkono Serikali ya Majimbo.

Lakini sio hii Majimbo ya wanasiasa wa Kenya ya ukabila ya kutaka makabila fulani wafukuzwe katika jimbo hilo. Ile federal

government kama ile ya United States of America, Canada na nchi zingine ambazo zimeendelea. Sitafafanua sana kwa sababu

itachukua muda lakini ijulikane kwamba maoni yangu ni kwamba naunga mkono Serikali ya Majimbo. Nije hapa nyumbani kwa

sababu mimi ni mtoto wa hapa nyumbani, ningependa kusema kwamba kwa sababu Katiba inahusu haki za watoto. Hapa tuna

makabila ambayo wanahamahama katika nchi yetu, zinaitwa pastoral communities. Kuna pengine Wa-Maasai, Wa-Rendille,

Borana, Wa-Somali na kadhalika. Ningependa Serikali au Katiba yetu ambayo tutakuwa tunatengeneza wakati huu, ichukulie

maanani makabila haya. Natumai Mwenyekiti wakati ulikuwa unakuja huku kwa gari, ukiangalia huko sehemu zimeachwa

kabisa.

Ningependa Katiba ichukulie maanani makabila yanayohamahama na wawe classified kama endangered species. Kama vile

tumesema ukimwi ni janga, tuseme pia makabila hawa, wawe endangered species na kuwe na Wizara maalum ambayo

itahusiana na hali ya kuchunguza haki ya makabila haya. Kuwe na Wizara katika Serikali ya kuangalia masilahi yao. Masilahi

kama elimu ya bure. Wawe hao watoto wanapewa chakula ya bure kama incentive. Kitu ya kuwaweka moyo wawe shuleni.

Wawe na free medical services au matibabu ya bure. Wakimaliza shule wawe wanapewa priority katika employment.

Wanapewa mstari wa mbele katika kuajiliwa ili wawe kama wale wengine na wawe pia kama incentive kuwapa moyo wale

hawajasoma ndio waweze kusoma. Na wawe wanapewa priority katika admission, katika enrolment. Hata saa ingine pengine

hawajafanya vizuri katika mitihani yao kwa sababu ya shida, kwa sababu ya ukame, sehemu wanaoishi wawe wanapewa

priority. Jambo lingine kidogo kugusia tu kwa sababu muda hautaniruhusu ni kwamba pia wananchi na wanyama. Hawa