constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
86

Administration yaani Chiefs. Chiefs wawe wanachaguliwa na raia kwa sababu tumekuwa na shida ya mtu kuchaguliwa na mtu

mmoja na kutaka atekeleze mapenzi yake mwenyewe na si masilahi ya mwananchi.

Jambo la pili ni kuhusu mwanamke. Mwanamke katika jamii ya Wa-Maasai hana haki, hawana haki, kwa sababu Maasai akioa

anaweza kumuacha yule mke wakati wowote anapotaka. Sasa Serikali kwa sababu hii Katiba inatengenezwa na wamama

Wa-Maasai wamepoteza maisha yao kwa sababu wanapoachwa na wazee hakuna kipengele cha sheria kinachowasimamia.

Maana kuna ndoa za kienyeji, zile za kawaida kinyumbani na huwa Serikali haitilii maanani hasa sana kwa upande wa jamii ya

Wa-Maasai, wamama wengi. Hata wengine wanapata stress na kufa. Maana wanafukuzwa wakati wowote na hawalipwi

chochote kutoka boma ile na labda amekaa miaka mingi akazaa na anafukuzwa, anaambiwa watoto ni wa bwana, mama

anaenda hana mtoto, hana mali, hana shamba. Kwa hivyo harithi chochote.

Kuhusu NGO’s zile ziko katika maeneo tofauti katika Kenya, ningependelea mimi kwa maoni yangu, Serikali iwe ikiingilia kati.

Kuweko na wakilishi kutoka kwa Serikali kwa sababu kumekuwa na mchezo ambao unachezwa ambaye kama NGO’s zikija

kuingia katika kufanya miradi, unakuta ni ya watu wachache, ndio wanaenda kufaidika nayo. Kwa hivyo ningeomba kwa mfano

kama Chiefs ama wakilishi kutoka Serikali, wawekwe katika kila sehemu ambayo NGO inafanya kazi.

Kuhusu afya, ningeomba Serikali iangalie kiasi cha umbali kutoka kwa kituo cha afya hadi kingine. Kwa sababu sikusema ziwe

chache lakini sehemu ile ambayo iko na mingi ni sawa hata kama ni baada ya nusu kilomita kuwe na kituo cha afya ni sawa.

Lakini kuna maeneo mengi hasa kama za jamii ambayo wanahamahama, unaweza kukuta hospitali karibu kilomita mia mbili ama

mia moja, uende ukakute kituo cha afya ambayo inaweza kusaidia wananchi. Na kuna mambo matatu ambayo Serikali ya

Kenya iliahidi wananchi kwamba watapambana na magonjwa na ujinga na ningeonelea kwa maoni yangu, kuwepo na kiasi ya

umbali ambayo Serikali itaangalia, kuwepo na kituo cha afya cha Serikali.

Kwa upande huo wa afya, ningependelea wale wahudumu wanaohudumu katika hospitali za Serikali wasiwe na biashara nje.

Kama mtu ni daktari na afanye huduma pale. Kuweko na hiyo sheria. Kama mtu anataka biashara, akafanye biashara na aache

ile maana kuna watu wengi wa Kenya ambao hawana kazi. Kwa sababu ukiangalia kama hospitali zetu hapa, unakuta madawa

zote zimeenda kwa ma-clinics za watu binafsi. Ukienda pale unaandikiwa rundo ya madawa, ukienda pale unakuta ni madaktari

wanauza zile madawa na kwa kweli imetuumiza sana.

Kuhusu ardhi: Ninaonelea ya kwamba kuna watu wanaona labda mbuga kama group ranches kwa mfano, watu wengi wanaona

wanafikiri ni sehemu ambazo hazina wenyewe ama hazina kazi. Lakini nigependa kusema tu kwamba hilo ni shamba la watu,

inaweza kuwa lina watu mia sita na hawajakatiwa bado na wana watoto wengi zaidi lakini bado hawajagawiwa kwa sababu

wanatumia kwa ufugaji. Ningeomba tu kwamba hata kama Katiba itapitisha kwamba, kuwepo na mahali ambapo Serikali ikatie

watu hawana ardhi. Lile ni shamba la wenyewe na lina idadi ya watu wake, wapewe nafasi ya kujisimamia wenyewe na

wapewe nafasi ya kujiandika wenyewe na hata kukaribisha mgeni kama atakuja alime. Lakini sio lazima awe mwenyeji eti kwa