constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
4

Watu wa Loitoktok, wanawakaribisha kwa moyo dhati kwa sababu haya mambo ya Katiba ni mambo ya maisha ya Wakenya.

Ama sivyo? Kwa hivyo nafurahia. Jana tulikuwa Rombo na kusema ukweli Wamaasai watu wanasema hawajasoma, lakini yale

mawazo walipeana nina uhakika hata wale wameenda University hawataweza. Na hiyo ni kwa sababu ya uongozi bora tukiwa

na Mheshimiwa, tukiwa na madiwani, tukiwa na wafanyikazi wa Serikali, viongozi wa dini, viongozi wa chama. Tumesema watu

wajulishwe katika kila sehemu kuja kupeana maoni yao kwa mambo ya Katiba. Kwa hivyo nafikiri wale Wamaasai tulikuwa

tunasema labda maoni yao itakuwa ni kasoro kwa sababu hawana masomo, lakini yale wamepeana, tunataka watu wa

Loitoktok, hata mvuje record zaidi. Kwa sababu wasomi si wako hapa?

Wale wasomi tunajivunia katika hii sehemu, si mko hapa? Kwa hivyo tunataka mpeane maoni yenu na mimi niko hapa

kukaribisha hao wageni. Baada ya kuwakaribisha nitakuwa raia mwema kama nyinyi. Msinihesabu kama D.O. Kwa sababu ni

lazima nije nisikize mambo ya Katiba. Leo niko D.O., kesho nitakuwa raia mwema kama nyinyi. Kwa hivyo ni kitu inahusu

maisha yetu. Kwa hivyo Bwana Commissioner, kwa sababu muda nao ni kidogo na watu ni wengi, na bado watakuja wengi.

Nasema karibuni Loitoktok na tunashukuru kwa nyinyi kufika, asanteni.

Com. Bishop Njoroge: Asante Bwana D.O. Sasa mimi nataka kuwaambia vile tutaendelea. Kwanza nataka kutangaza kikao

hiki kama kikao rasmi ya Katiba na tunapoketi hapa tujue tuna sheria ile inayo tusimamia kwa yale mambo ambayo tutafanya

hivi leo. Jambo la kwanza, kila mtu atakuwa huru kusema maneno ambayo anafikiria inaweza kusaidia katika kuunda Katiba.

Kama mjuavyo, Katiba hii ni watu wenyewe waseme wanataka iwe namna gani. Kwa hivyo msiogope kwamba D.O. yuko

hapa. Hata wakati tuna P.C au Mawaziri wa Serikali, wanajua kwamba watu ni lazima wawe huru kusema yale wanayohitaji

kusema. Hakuna mtu anaweza kufuatwa kwa sababu ya yale aliyoyasema leo. Ile Act ambayo inatutawala inasema, kila mtu

ana uhuru. Lakini ningetaka kusema hivi; hakuna mtu ana uhuru kuzungumza juu ya mtu binafsi kwa njia yeyote mbaya ama

njema. Kwa sababu ni Katiba tunafanya nini? Tunatengeneza. Ninataka kutoa mfano. Mtu anaweza kusema, tunataka mamlaka

ya Rais ipunguzwe. Haya ni mapendekezo, inafaa. Lakini huwezi kusema juu ya mtu katika Serikali kwa njia yeyote mbaya kwa

sababu hiyo haitaenda katika Katiba. Tumekubaliana hivyo? Na mtu akisema hivyo, nitamkataza kuendelea kwa sababu ni

lazima tuwe na mapendekezo ambayo yataingia kwa Katiba. Unaweza kuwa na Mbunge na huna furaha naye, huna ruhusa

kusema juu ya Mbunge. Unaweza kusema tunahitaji barabara. Sawasawa? Hayo ni mambo ya Kikatiba. Kwa hivyo hata kama

tuna uhuru, hatuna uhuru wa kusema mabaya ya watu. Si hapo tumekubaliana?

Jambo la pili, sisi ni Wakenya, tunajua kuna shida nyingi. Tunajua kuna watu wengi hawana pesa ya kwenda kununua madawa.

Tunajua mara ingine kwa mahospitali hakuna madawa. Kwa hivyo usituambie zile shida kwa urefu, tuambie mapendekezo yako

ni nini, ili tutatue shida gani? Shida hiyo. Tukifanya hivyo, tutatumia muda mfupi na yale ambayo unasema, itasaidia kutengeneza

Katiba hii. Kwa hivyo tunataka mapendekezo. Kama jana, kama vile D.O. alivyosema na Councillor pia alisema vizuri huko

Rombo kwamba tunahitaji tu mapendekezo. Kwa sababu hiyo ndio itaenda kwa Katiba.