27.11.2014 Views

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

56

mbao kabla ya miti kuwa imetoshea. Ningeomba kuwe na sheria kali ambayo mtu ataadhibiwa, hata awe ni Rais, awe ni nani,

aadhibiwe kama anapeana ruhusu ama amepatikana akipasua mbao katika forest. Sehemu za chemchem ya maji ama mito,

kando kando ya maji, ningependekeza kuwekwe sheria, mtu ambaye shamba yake imekaribia kwa maji, at least hatua fulani

ziwe ni za miti, sio za kulimwa, ikabe hiyo maji.

Kwa mfano katika hii sehemu yetu ya Nodrues, watu wale ambao wanaishi hiyo sehemu, ingetengwo hiyo ardhi iwe ni water

catchment na ipandwe miti na wale wako hapo wahamishwe wapewe shamba mahali pengine ambao ni pazuri kama hapo.

Lakini wale watafutiwe mahali kwa sababu wataharibu maji, kwa sababu mwanzo wata-pollute hiyo maji na tena watafanya

ikuje kukauka haraka. Kwa hivyo national resources ni lazima zitunzwe kwa njia ya hali ya juu. Pawe na sheria inasimamia

hivyo. Asanteni.

Com. Bishop Njoroge: Elijah Ole Koptitat, akifuatwa na Simon Gachuru. Simon Gachuru yuko?

Elijah Ole Koptitat: Mimi ninaitwa Elijah Koptitat, sio Peter. Yangu ya kwanza ni juu ya Rais. Rais awe ni mtu ambaye

anachaguliwa na watu wote. Waziri Mkuu pia nafasi yake ipatikane. Nafasi ya Waziri Mkuu pia ni nafasi ambayo ingefaa

ipatikane. Mbunge achaguliwe mtu ambaye amemaliza form 4, isiwe chini ya form 4, form 4 na juu. Pia nominated MPs kuwe ni

mama au mlemavu. Asiwe ni mtu ambaye ni mwanamume anaweza kwenda kujitafutia kura. Lakini maana mama hawezei

kutembea sana, labda anaolewa. Au mlemavu hawezi kutembea kwa hivyo ningesema hiyo nafasi ya nominated MP, iwe ni ya

akina mama na walemavu.

Councillor awe pia ni mtu wa form four and above. Asiwe tena mtu wa chini wa Primary school. Provincial Administration

idumu kama kawaida. Iendelee tu kama kawaida lakini ningeomba kwa nafasi ya Ma-Chiefs, Chief awe ni mtu wa kutoka pia

naye O’level na kuendelea juu. Asiwe chini ya O’level. Na pia awe anachaguliwa na wale watu wa hiyo location anayotaka

kusimamia. Maana hii kazi ya kwenda interviews huko kwa wilaya, saa ingine inachaguliwa mtu ambaye hafai kabisa. Kwa

hivyo ingefaa kabisa awe anachuguliwa na wale watu wake wanaotaka kumsimamia. Mambo ya national parks iwe chini ya

Local Aauthority kama game reserves kwa hivyo isiwe tena chini ya Central Government.

Serikali, mimi kwa maoni yangu ningependa Serikali ya Majimbo kabisa. Serikali ya Majimbo ianzishwe hasa kutoka uchuguzi

huu ambao tunaenda sasa.

Land Control Boards: Mashamba yauzwe na familia nzima na sio mzee tu au mama kama hana bwana. Awe ni mama tu

mwenyewe anaenda kuuza shamba kwa sababu ana familia mwenyewe. Iwe inauzwa na familia nzima, wakubaliane na wote

waende kwa Land Control Board waseme ya kwamba, tumekubalia kwa ajili ya hili tatizo na hili basi lipewe kwanza.

Com. Bishop Njoroge: Wacha nikuulize kabla hujafika hapo. Huko Kimana, tuliambiwa kwamba ili kuzuia kuuzwa kwa

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!