constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
62

Com. Bishop Njoroge: Jiandikishe pale. Josephat Kilingu? Ningetaka kuwaambia sasa tuzungumze kwa haraka. Tuna listi ya

watu mia moja thelathini na sita na tumefikia tu namba hamsini na nne. Kwa hivyo mnaona ni watu wengi. Msipofanya haraka,

kuna wengine hawatazungumza.

Josephat Kilungu: Nashukuru sana kwa kupata nafasi hii. Kwa majina yangu ni Josephat Kilungu kutoka shule ya upili ya

Ilasit. Niko hapa kutoa maoni yangu kuhusu.

Com. Bishop Njoroge: Which form are you in?

Josephat Kilungu: Form four.

Com. Bishop Njoroge: How old are you?

Josephat Kilungu: I am twenty-two years. Nimekuja hapa kutoa maoni yangu kuhusu Katiba ya Kenya. Kwanza kabisa

ningependa kuzungumza kuhusu masomo ya shuleni. Kwa kweli kabisa kama sisi wanafunzi tunaumia sana kwani masomo

shuleni yamekuwa mengi sana kiasi kwamba yanatuchosha. Kwa hivyo kama ingewezekana ni vyema kama masomo

yangepunguzwa. Masomo yapunguzwe yawe angalao hata kama ni tano, halafu wanafunzi ndio waweze kupata nafasi ya

kusoma masomo hayo. Pia katika shule, mashule mengi humo nchini, kuna wazazi ambao ni maskini ambao hawawezi

kuwafundisha wanafunzi au hawana fedha za kuwafundisha wanafunzi wale. Kwa hivyo ni vyema kama Serikali ingetoa msaada

wa fedha na pia vyakula katika mashule yetu. Ndiposa, wale wazazi ambao hawawezi kuwahitimu wanafunzi wao kifedha ama

kivyakula, wafaidike katika masomo yetu pia.

Pia, kuna mashule ambazo zimechanganyikana. Kuna shule zetu Kenya, zile shule zinafanya vizuri unakuta ni shule ambazo ni za

wavulana peke yao ama wasichana peke yao. Kwa hivyo ningependa Serikali yetu iweke shule zote ziwe, kama ni za

wasichana ziwe - za wasichana peke yake. Kama ni za wanaume, basi ziwe za wanaume peke yake. Hizi shule za

mchanganyiko, zisiwe kabisa katika nchi yetu. Kwa sababu ukiangalia, shule zinafanya vizuri ni hizo.

Com. Bishop Njoroge: Don’t explain. Go straight to the point.

Josephat Kilungu: Pia ningependa mashule yapewe magari kwa sababu shule nyingi ziko na shida za usafiri. Kwa hivyo ni

vyema Serikali kama ingepata magari ya kusafiria huko shuleni. Pia tungependa Serikali kama ingepeana mafunzo kuhusu

Katiba. Mambo kama haya ya Katiba kuna mashule mengi sana hayajui mambo ya Katiba. Kwa hivyo ni vyema kama

tungepata mafunzo ya Katiba huko shuleni. Pia mafunzo kuhusu afya ni vyema. Magonjwa kama haya hatari hatari, ni vyema

kama Serikali ingetupatia mafunzo kuhusu haya magonjwa. Tungefurahia sana. Pia kuna haya masomo ya computer. Ingekuwa