constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
85

Koyan Ole Masunga: Ingine, tuko na shida na tunashukuru hii Katiba kwa maana tuko na mahospitali. Serikali ya ukoloni

zamani ilikuwa ya bure. Tumepata uhuru wetu na ni kama hayo mambo imekuwa mabaya.

Com. Bishop Njoroge: Ungetaka hospitali iwe ya bure?

Koyan Ole Masunga: Tungetaka hospitali iwe ya bure.

Com. Bishop Njoroge: Kwenda nyingine.

Koyan Ole Masunga: Madaktari wanyimwe zile hospitali zao za nje. Ingine ya tatu ni ya mashule. Mashule nayo pia, wakati

wa ukoloni, mkoloni alikuwa anasomesha watoto na sasa Serikali yetu sasa, (inaudible). Kwa hivyo tunataka masomo ya bure.

Hakuna Serikali na Serikali.

Ya nne, upande wa Agriculture. Agriculturist, hawafanyi kazi yao. Tunasikia jina tu agriculturalist lakini hatumuoni. Kulinda miti

yote ilikuwa imekatwa na huyu mtu alikuwa, kwa hivyo wao hawafanyi kazi. Kwa hivyo nchi imekuwa jangwa kwa vile wale

waliokuwa wanalinda hiyo misitu, hawalindi.

Upande wa veterinary: Naye veterinary pia, zamani wakati wa mkoloni, walikuwa wanaangalia mifugo yetu lakini sasa

hawaangalii ni jina tu veterinary ni sisi tunasimamia mali yetu. Kwa hivyo nayo Serikali iangalie.

Ya tano, tunataka Majimbo. Sio Majimbo ya mtu ahame mwenye alikuwa amehamia hapa. Tupewe Majimbo lakini tulinde mali

yetu na tuangalie hasara na faida. Wakulima wamekuwa watu wa bure. Hakuna faida yeyote tunapata. Tunataka Serikali

iangalie bei ya mkulima maana mkulima ni kama mtu amefungwa na mkulima kama anakwama, hata Serikali haiko. Kwa hivyo

mkulima aangaliwe sana. Mambo ya kibarua, kibarua iko juu lakini mavuno yako chini.

Com. Bishop Njoroge: Mzee, nenda kwa pointi yako ya mwisho.

Koyan Ole Masunga: Pointi yangu ya mwisho, Serikali yetu tukufu, Rais wetu awe na kipindi cha miaka kumi. Wabunge

wetu wawe na kipindi cha miaka tano kama kawaida. Wabunge wetu, zile pesa wanamwaga mwaga ovyo ovyo, aje amwage

kwa mashule. Sio kuja kununua watu. Asante.

Com. Bishop Njoroge: Rev. Simon Kanaiya? Karibu.

Rev. Simon Kanaiya: Majina yangu ni Rev. Archdeacon Kanaiya na mimi ni mkaaji wa hapa Loitoktok na nimeshukuru sana

kupata nafasi hii kujadili juu ya Katiba ambayo ndio inaangalia masilahi ya Kenya. Jambo la kwanza ni kuhusu mambo ya