constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
63

ni vizuri sana kama computer lessons zingekuwa compulsory kwa kila mwanafunzi. Kwa sababu kuna mashule mengi hawana

computer. Kwa hivyo ni vizuri kama ingekuwa compulsory kwa kila mwanafunzi.

Pia usalama shuleni. Mashule mengi hayana usalama. Ni vyema kama Serikali ingepeana usalama huko shuleni ili mambo kama

kuchomwa kwa wanafunzi, kesi kama hizo ziishe. Pawe na usalama. Masomo kama ya hesabu ama haya ya science, masomo

haya yamekuwa magumu sana na hapo mbeleni ukiangalia ni vyema, watu walikuwa wanafanya vizuri haya masomo. Kwa hivyo

inamaanisha kuna jambo fulani ambalo limefanya au vitu vimeongezwa, haya masomo yakawa magumu mno. Kwa hivyo ni

vyema kama ingerahisishwa ili angalao wanafunzi wawe wakipita maana mbeleni walikuwa wanapita lakini sasa hawapita.

Kumaanisha ya kwamba kuna vitu ambavo viliongezwa huko ambazo zinasababisha wanafunzi waanguke.

Com. Bishop Njoroge: Unasema standard iletwe chini ili wanafunzi wapite?

Josephat Kilungu: No.

Com. Bishop Njoroge: Sema yako ya mwisho.

Josephat Kilungu: Langu la mwisho, Muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashiriki. Ingekuwa ni vizuri sana, wakati viongozi

wanakutana kwenda kutoa maoni yao katika Muuongano wa East Africa, ni vyema pia kama wanafunzi wangepewa nafasi

wanashiriki katika hiyo mikutano ndio tujue ni nini inaendelea. Kwa hayo machache, nashukuru sana.

Com. Bishop Njoroge: Thank you very much. Very clear thinking, come here and register. I wish you well in your studies.

Tupate Esther Wangechi. Karibu.

Esther Wangechi: Nashukuru sana kwa nafasi hii ambayo ninakuja kutoa maoni yangu kuhusu Katiba. Jina langu ni Esther

Wangechi kutoka shule ya upili ya Ilasit. Kwa maoni yangu, ningependa katika kila shule kuwe na hii ofisi ya guiding and

counseling. Ukiangalia wanafunzi wengi, wengine wanaacha shule kwa kukosa mawaidha.

Jambo la pili shule ziongezwe. Shule na pia waalimu waongeze ili elimu katika mashule iwe bora. Jambo lingine ni, ukiangalia si

wazazi wote wana uwezo wa kuwasomesha vyema watoto wao. Kwa hivyo ningependelea Serikali ipeane kama ni bursaries za

shule na pia vitabu hizi za textbooks ili wanafunzi waweze kufaulu vizuri.

Jambo lingine ni elimu ya wasichana. Wanafunzi wasichana wapewe nafasi ya kusoma katika viwango vyote vya elimu.

Ukiangalia wanafunzi wengi hawamalizi shule maana wanaozwa. Jambo lingine ni usawa wa vifaa katika mashule. Ningependa

mashule yote yawe na usawa wa vifaa. Si kwamba mashule mengine ni bora kuliko mengine. Kwa mfano katika maabara, vifaa

viwe sawa katika shule zote.