constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
12

itarudishwa kwetu tukiona ya kwama yeye hafai. Na kwa hivyo tutarudishiwa na wananchi watapewa maoni yao. Wakishatoa

yale maoni, yale maoni ndio yatapelekewa wale Ma-MP na vote of no confidence ambayo itakuwa ni fifty five percent.

Ikipitishwa basi yule President anatoka na tuna-elect another President.

Huduma za lazima: Huduma za lazima ni kama elimu, health na kadhalika. Sasa katika huduma za lazima, kwanza katika elimu.

Elimu ni muhimu katika nchi na kwa hivyo, lazima elimu iendelezwe na wale ambao ni professional. Sio mtu tu ambaye hawezi

kuendeleza elimu. Wanasiasa wameachiwa mamlaka mengi sana katika kuendeleza elimu. Kwa mfano tukichukua 8-4-4,

ilikuwa ni elimu mzuri lakini kwa sababu wanasiasa waliingilia, wa leo utakuta kwamba inaonekana ni kama sio chombo

ambacho kilikuwa ni cha muhimu. Na ingali ilikuwako ni kumsaidia yule mtoto, akitoka nje iweze kumsaidia katika pande

mbalimbali. Kwa hivyo maoni yangu ni kwamba professionals waachiwe ku-draw the curriculum na waachiwe pia kuendeleza

katika elimu. Pia health hivyo hivyo.

Biashara zimewekwa vikwazo vingi sana. Lazima uwe na licence, pia kodi ziko nyingi nyingi na hizo kodi utakuta ya kwamba

yule, kama ni kijana ama ni mzee ambaye amekuwa retrenched or so, hawezi akaendeleza ile biashara kwa sababu ile kodi

iliyoko ni nyingi sana. Kwa hivyo kodi iondolewe katika pande za biashara na hata ikiwa ni katika mambo ya kutoa vitu hivi,

kama ni biashara kidogo kidogo, mama anakwenda jikoni kununua vitu vidogo vidogo, hizo biashara zimewekwa kodi ya aina

yeyote, ziondolewe.

Com. Bishop Njoroge: Bwana Philip, umetumia dakika kumi, nakupatia dakika moja.

Philip Leshinka: Sasa tunaanza mashamba. Mashamba wakulima wapatiwe mbegu kwa sababu ukulima ni uti wa mgongo

katika nchi hii. Wapatiwe mbegu na chemicals za kuweza kuondoa wadudu na kadhalika. Pia soko wakulima wapatiwe.

Halafu jambo la mwisho ni juu ya mazingira. Mazingira ni jambo la muhimu zaidi na ni lazima kila mtu ahimiziwe kuweka

mazingira safi. Kama ni mambo ya ukataji wa miti, ukataliwe mbali, kama ni mambo ya kwenda kulima kando kando ya mito,

ukataliwe mbali. Kama ni mambo ya kuenda kukata miti, pahali ambapo vianzo vya maji zipo, ukataliwe mbali. Na ni hayo tu.

Com. Bishop Njoroge: Tupate Bernard Kamau.

Bernard Kamau: Asante sana kwa kunipa muda wa kusema. Kitu cha kwanza, pesa ya Serikali inatakiwa itoke kwa Bunge.

La pili, jina ukabila lipigwe marufuku hata ikiwa ni kwa mkutano. Ya tatu, tunatakiwa tuwe tukiuliza maswali kwa mkutano. Ya

nne, Kenya inatakiwa kuwe na vyama vitatu. Ya tano, Mbunge angetoka chama hiki, aende chama kingine, kusifanywe

uchaguzi tena, kukae namna hiyo. Yangu ni hayo.

Com. Lethome: Neno ukabila umesema liwe katika mkutano? Hebu fafanue.