27.11.2014 Views

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

43

Com. Bishop Njoroge: Kwa hivyo ungetaka ikae au iondolewe?

John K. Gichia: Enquiries ziendelee lakini zisikae muda mrefu.

Com. Lethome: Matokeo yake, ungependa yatangazwe kwa watu ama iwe siri ya Rais?

John K. Gichia: Hatutaki iwe siri ya Rais. Kama ni mambo kama kifo cha Ouko, ambao watu wengi walilia kujua. Hatukujua

nani aliua? Labda mpaka saa hii wanajua. Tungependa tuwe tukiambiwa wazi.

Ya mwisho, nasikia kuna watu wanasema mambo ya Administration iondolewe kama Chief. Mimi ningeonelea Administration

yote, ikae hivo hivo. Security pia ambayo iko nchini, iendelee hivyo hivyo. Kwa sababu sioni sababu uondoe Chief. Labda

anayelalamika Chief aondolewe, labda ni mkatili katika eneo lake. Kwa hivyo naomba Administration ikae hivyo hivyo.

Asanteni.

Com. Bishop Njoroge: Asante John. Tupate Samuel Nyaoga. Medingi Ole Mlaroni. Karibu Mzee. Taja jina lako kwanza.

Medingi Ole Mlaroni: Mimi kwa majina naitwa Medingi Ole Mlaroni. Mimi ni Mzee ambaye anaishi sehemu ya Ole Leti,

katika sehemu za Rongai. Mimi naeleza mapendekezo yangu; ya kwanza napendekeza Raisa awe na uwezo wa kusimamia

Kenya mzima. Halafu pendekezo la pili, ninapendekeza ya kwamba, Kenya iwe na Serikali ya Majimbo lakini iwe Rais ndiye

anasimamia wote.

Pendekezo langu la tatu ni kwamba katika sehemu ya Wa-Maasai. Kuna sehemu nyingi imeenda kama Amboseli. Kama

sehemu hiyo ambayo ilikuwa inaitwa Tsavo. Irudishwe iwe mikononi ya wenyeji.

Jambo lingine la tatu ni kwamba masomo katika sehemu ya Wa-Maasai inakuwa dhiifu kidogo. Ningeomba Ma-Chief wapewe

nafasi, kabisa waweze kuwa na sheria ya kusema watoto wapelekwe shuleni. Kwa sababu tunaona masomo siku hizi ndio kitu

kikubwa ambacho unaweza kumuachia mtoto wako. Kwa hivyo Ma-Chief, mimi napendekeza Ma-Chief wachukue sheria

hiyo, iwe ni sheria katika nchi ya Wa-Maasai ama katika Kenya.

Jambo lingine Councillors: Ma-Councillors ambao wanachaguliwa katika Kenya, wao wenyewe wanachukua madaraka yao na

hakuna kitu anaweza kuwapa wananchi sawasawa kulingana na vile inatakikana. Iwe plots, Councillor awe na kamati yake,

ambayo inatoka katika ile eneo ambayo inasimamia Ward yake ili wakae na kugawa zile plots. Isiwe anakuja na agawie watu

wale anawapenda. Anaweza kuwa anagawia ndugu yake ama anagawia mtu ambaye alikuwa rafiki yake. Kwa hivyo tunataka

Councillors wawe ni watu ambao watakuwa na kamati ambayo itasimamia plots.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!