constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
68

Translator: Kwa hivyo ni hayo tu. Asanteni.

Com. Bishop Njoroge: Mama njoo pale. Unasikia wanaume sasa tuko katika shida. Njoo hapa Mzee.

Samuel Kahiu: Jina langu ni Samuel Kahiu. Nikichangia mjadala huu wa Katiba, tunaona Ma-Chifu watu wakichaguliwa kama

zamani. Ma-Chifu wawe wakichaguliwa na raia kama zamani wakati wa enzi ya Mzee. Mwananchi wa Kenya ana haki ya

kukaa pahali popote anataka kukaa na akimaliza kama miaka ishirini, awe akigombania kiti chochote, akiwa ni Chifu, akiwa ni

Mbunge, awe akigombania maanake watoto wale wamezaliwa hapo wamekua na wakuwa watu wakubwa. Kwa upande wa

wananchi, mwananchi wa Kenya apewa heshima kama watu wale wengine kama Wahindi, Waarabu, maana ukiangalia kama

mtu anaitwa Mwarabu, anaweza kupiga mwananchi wa Kenya na asiulizwe na mtu.Maana yake mwananchi wa Kenya hana

nafasi ya kujitetea maana ni pesa inaingia.

Kitu kinaitwa Majimbo, hiyo itupiliwe mbali. Maanake kuna kufunikwa kwa watu (inaudible). Na hii Majimbo ndio huleta utata,

ukiangalia kama Uganda, kwingineko kuko na uchacha shauri ya hii Majimbo. Watu wale mia nne, watu wale wana taabu,

hawapatiwi pesa ya kuridhisha. Wapatiwe pesa ya kuweza kuenda kuangalia kazi yake maana sasa ameacha kazi.

Madiwani: Madiwani wale wanateuliwa, wawe wakiteuliwa juu ana masomo. Kwa hivyo sina mengi ni hayo tu.

Com. Lethome: Asante sana Mzee Samuel. Julius Ntei Korati yuko? Simon Maritei? Lawrence Karanja. Muteli Minduti,

Tepai Tapokoi, James M. Wahome. Karibu Wahome. Joseph Kiutho yuko?

James Wahome: Kwa majina ni James Mburu Wahome. Yangu ninapendekeza Rais awe anachaguliwa na wananchi wote

bila kutoka kwa chama chochote na awe hana mamlaka makubwa kama hiyo ya kuteua wasimamizi wa sehemu hizo za kama

Ma-Judges na wale wengine ambao wanasimamia hata kama ni kuchagua hao wasimamizi wa vyuo vikuu. Wawe

wanachaguliwa kupitia kwa Parliament. Pia ninapendekeza wanaochagua wawe na uwezo wa kupitisha vote of no confidence

na Mbunge wao kama hawatendei vyema.

Pia ninapendekeza habari ya mashamba. Kwa kweli tuna watu ambao wana mashamba vikundi vikundi ama hapa na pale na

bado ana shamba moja kubwa ambayo haitumiki. Unasikia mtu ana acre elfu ishirini na tano na hali kuna mwananchi ambaye

hana hata chochote. Ninafikiria iwe ni haki ya mtu yeyote katika Kenya apate ardhi. Pia ninapendekeza iwe ni haki ya masomo

kwa kila mtoto ama yeyote yule ako Kenya. Iwe ni haki. Upande huo wa masomo kutoka kiwango cha chini mpaka cha juu,

Serikali iwe inaangalia. Kama ni hao walimu wapate mishahara mikubwa na kwa njia hiyo tutaepusha hawa watu wa chokora

na hao watu wengine ambao tunaona hawana elimu. Kufikia hapo, ninaona iwe ni haki ya mtu kuishi popote pale na ikiwa ana

rasilimali mahali pale anaishi, awe na haki pia ya kugombania kiti chochote kile cha utawala. Kwa hayo machache asante.