constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
57

mashamba kwa njia hiyo, mama na mzee wawekwe katika Title Deed. Kwa sababu hiyo itazuia mzee kuuza kama mama hajui.

Hata mzee mwingine alisema mama, mzee na watoto waingizwe katika Title Deed. Ungefikiria namna gani?

Elijah Ole Koptitat: Ardhi: Kuna ardhi ambayo inataliwa na mtu anaitwa Commissioner of Lands. Mimi kwa maoni yangu

ningesema ya kwamba, iwe inaangaliwa iko chini ya wenyeji wa hapo hapo na sio Commissioner of Lands maana huyo anauza

bila wenyewe kujua ardhi imeenda wapi.

Elimu: Elimu iwe ni ya lazima kwa watoto wote, wavulana kwa wasichana na iwe ni ya lazima. Watoto wakifika umri wa

kwenda shuleni, mtoto aende kwa lazima shuleni na elimu iwe ni ya bure. Pia mzazi au mtu yeyote akitoa mtoto wa kike shuleni

kwa njia ya kwenda kuoza au mtoto wa kike akiwekwa mimba au kutoa tu mtoto wa kike kwa njia yeyote, huyu mtu

ashitakiwe mara moja. Pia nafasi, intake ya Teachers Training Colleges, watoto wa sehemu kame, wafikiriwe kwa upande wa

marks. Maana labda hawatakuwa sawasawa na watoto wa miji. Kwa hivyo mimi ningeomba watoto wa sehemu kame

wafikiriwe wakati wa kupelekwa katika Teachers Training College.

Uongozi katika sehemu mbalimbali: Uongozi uwe mikononi mwa wenyeji wa eneo fulani. Kwa mfano Chifu, Councillor na

Mbunge, mtu ambaye ni mgeni aliyekuja kutoka mbali, aje kutafuta U-Chifu hapa katika sehemu ambayo yeye ni mgeni

kwanza. Au Councillor aje kutafuta kazi ya Council hapa, wangepatiwa nafasi wenyeji, Chiefs, Councillor na hata Mbunge

lakini sio mgeni. Kazi pia ya Serikali.

Com. Bishop Njoroge: Sheria ambayo inatutawala inasema Mkenya ambaye yuko mahali fulani, huwezi kumnyima haki kuwa

katika cheo fulani. Sasa unataka tubadilishe hiyo sheria sasa tuseme kila mahali, mtu ambaye hajazaliwa hapo, hawezi kupata

cheo fulani katika mahali pale?

Elijah Ole Koptitat: Ndio sababu Bwana Commissioner tuko hapa tunabadilisha. Tunataka tubadilishe. Kazi ya Serikali

ifikiriwe wenyeji wa eneo hilo kwanza. Kwa mfano kazi ikipeanwa interviews, watu ambao ni wa nje ndio hupatiwa zaidi kwa

ajili inasemekana ya kwamba ndio wana market zaidi. Kwa hivyowatu wa area hiyo hiyo hata kwa kazi ya Serikali, kwa

interviews first priority iende kwa wenyeji.

Ya mwisho, ni watu kujipatia majina ya mahali ambapo sio kwao kwa ajili ya kutafuta kazi au kupita mitihani. Kuna watu wengi

ambao katika nchi hii yetu ya Kenya wana majina ambayo si ya kwao. Lakini kwa ajili ya mitihani, ili waende Secondary

schools au University au kazi, wanasema mimi ni Ole. Na kumbe sio Ole, yeye ni wa mahali pengine. Lakini kwa ajili ya kupata

kazi, anajipatia jina la bandia. Kwa hivyo imi yangu ningesema ya kwamba, mtu achukue jina la kwao na kama hiyo ni riziki ya

kazi kutoka kwa Mungu, atapata tu hiyo kazi. Kwa hivyo, mimi hayo ndio yangu.

Com. Bishop Njoroge: Asante Bwana Koptitat kwa maoni hayo. Njoo hapa ujiandikishe katika register. Tukimaliza na huyu