constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
54

Unaenda pale, yeye ndio anatatua kesi na hiyo kesi ingekaguliwa tu na elders wa eneo hilo.

Tukija upande wa hospitali: Hospitali ziwe za bure, maji iwe ya bure na education. Kwa ajili watu wengi wameshakuwa maskini

kabisa kwa ajili mkulima analima shamba, Serikali haitilii maanani huyo mkulima, chakula yake anatoa. Hajui specific price

anaenda kuuza bei gani. Akikula leo mahindi ni shilingi mia tatu, mtoto anatakiwa elfu ishirini na tano Sekondari, kwa hivyo

elimu iwe ya bure.

Madaktari waongezewe mishahara na wanyimwe kufungua clinics. Ukienda especially our district hospital here Loitoktok,

unaenda unaambiwa hakuna dawa, nenda clinic fulani. Na unakuta the same medicine imetoka kwa hiyo hospitali kubwa na

ikaenda kwa hiyo. Kwa hivyo madaktari waongezewe mishahara, wasiwe na biashara yeyote ya hospitali ndogo ndogo kando

ya hospitali kubwa kubwa.

Group ranches at least isimamiwe na wenyeji na iwe na auditing kwa ajili hizi pesa tunapewa na K.W.S haitoshi. Tunataka

iongezwe na iwe na auditing ijulikane hiyo hela kama ingesomesha watoto au ingetumiwa na individual. Unakuta mtu ameenda

kununua gari, amenunua (inaudible) zake, unakuta hizo hela hazi-educate wale members wa group ranches, unakuta ina-educate

mtu fulani kwa ajili ni Chairman. Especially unakuta wengine walikuwa wanasimamia group ranches, they are not helpful for the

area. Unakuta anapewa pesa ya kwenda kusoma kwa masomo ya juu na ingali watoto native, wako nyumbani hawajasoma na

hawajapewa hela ya kuwasaidia. Ni hayo tu.

Com. Bishop Njoroge: Thank you Mr. Kulare. Francis Wambua? Akifuatwa na Paul Njenga. Paul Njenga yuko wapi? Peter

Koptitat yuko? Unamfuata.

Francis Wambua: Asante sana. Kwa majina naitwa Francis Wambua na mimi ni mfanyikazi wa sehemu hii ya Loitoktok.

Ningependa kutoa maoni yangu juu ya hii Commission. Mwanzo ningependa kuangalia katika uchaguzi wa MPs na Councillors.

Nikianzia na uchaguzi wa Rais, Rais angechaguliwa bila kuwa MP mahali popote. Achaguliwe asimame tu kama mtu kwa kiti

cha Rais peke yake. Ili asikuwe mtu wa kupendelea sehemu yake aache sehemu ya nchi yake. MPs nao wachaguliwe watu

ambao wamesoma hasa kwanzia kidato cha Form four. Wawe na elimu ya kutosha, sio watu wa kwenda kulala kwa Bunge,

kuchukua mishahara mikubwa bure. Tukiangalia tena wangetakiwa wakae kwa miaka mitano ili uchaguzi ufanywe tena.

Ya pili ningependa kuongea juu ya Land issues: Ardhi ya Kenya ingetakiwa kuwa ni ardhi ya Serikali na mwananchi kama

angekuwa na kubwa, aruhusiwe kuwa tu na less than fifty acres. Akiwa na zaidi ya hiyo anyang’anywe, ipewe wale ambao

wanaihitaji ambao hawana land na waendeleze. Kama mtu amepewa na hawezi kuendeleza, ichukuliwe ipewe mwingine

anaweza kuiendeleza.

Kabla hujatoka hapo, tumeambiwa hapa kuna watu kama Wa-Maasai ambao ni wafugaji na wanahitaji ardhi kubwa katika